Sambaza:

Msanii wa muziki, Vanessa Mdee anayefanya vizuri katika soko la muziki nchini Tanzania ameendelea kuwa na wiki ya kihistoria ambayo ilianza kwa kuzindua albamu yake mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wake na wadau wengine wa mziki nchini siku ya Jumatatu. Kesho Jumamosi ya January 20 2018 ndio CD za abum yake ya Money Mondays zitakuwa zinatoka.

Vanessa Mdee

Ijumaa hii Vanessa amezindua programu ‘app’ yake mpya ya simu ya VEE MONEY ambayo inapatikana bure kupitia ‘Google Play store’ na ‘Apple store’. Programu hii ambayo imetengenezwa na kampuni ya masuala ya teknolojia ya Marekani, Converge Media, ni sehemu ambayo mashabiki wa Vanessa watakuwa wanapata maudhui ya kipekee ya Vanessa kama vile; nyimbo, video, picha, na kuona kurasa zake za kijamii

SOMA NA HII:  SUA kuokoa asilimia 40 ya mazao yanayoharibiwa na panya shambani

‘Kwanza natoa shukrani za dhati kwa mashabiki wangu kwa kuipokea albamu yangu kwa mikono miwili, na sasa natumaini app hii itazidi kutuweka karibu,” alisema Vannesa.

Programu hii imetengenezwa na kampuni ya masuala ya teknolojia ya Marekani Converge Media, lengo likiwa ni kutengeneza sehemu ambayo mashabiki wa Vanessa watakuwa wanapata ya kusikia/kuona video, nyimbo, picha na kurasa za kijamii za muimbaji Vanessa Mdee.

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako