Nyingine

Uwanja wa ndege wa Madeira umebadilishwa jina na kuitwa Cristiano Ronaldo

Ronaldo leo amehudhuria Madeira katika sherehe za ubadilishwaji wa jina la uwanja wa ndege wa kimataifa wa Madeira na kuitwa jina lake kwa heshima, sherehe ambayo imehudhuriwa na watu mbalimbali Madeira wakiwemo mashabiki.

Ronaldo ambaye alizaliwa 1985 katika mji mkuu wa Madeira, Funchal na baadaye akachezea Sporting Lisbon na Manchester United. Maamuzi ya uwanja wa ndege kupewa jina lake, yamekuja kutokana na kupewa heshima kutokana na jitihada zake ambazo amezifanya katika mchezo wa soka na jina lake kuitangaza vizuri Madeira.

“Wakati mwingine, shukrani za taifa huwa hazidumu sana, lakini Madeira haitasahau,” Miguel Albuquerque, rais wa serikali ya Madeira alitangaza, hatua ya kubadilisha jina la uwanja huo ilipotangazwa.

SOMA NA HII:  80% watashindwa mchezo huu: ni Glass gani itajazwa kwanza?

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published.