UTAFITI: Vyakula vya kuokwa husababisha magonjwa haya


Wataalamu wa afya duniani na tafiti mbalimbali zimeeleza aina mbalimbali za vyakula ambavyo huwa na madhara na jinsi gani vinaweza kuepukwa na mtu kuepuka kupata magonjwa mbalimbali kwa kula na kuishi kwa afya.

Hivi karibuni watafiti kutoka nchini Ufaransa wameleeza kuwa vyakula vya kuokwa humweka mtumiaji kwenye hatari ya kupata magonjwa ya saratani.

Wametaja baadhi ya vyakula hivyo kuwa ni pamoja na keki, kuku na nyama, mikate na vinginevyo kwasababu ni vyakula ambavyo kabla havijaokwa huwekewa vitu kama mafuta mengi, sukari, viungo mbalimbali ambayo ndio sababu ya kupelekea saratani.

Wataalamu hao wameeleza kuwa kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya vyakula hivi miaka ya hivi karibuni, kuna uwezekano wa ongezeko kubwa la magonjwa ya saratani katika miaka 10 ijayo duniani kote.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA