Nyingine

Utafiti mpya unasema nusu ya vijana wa Afrika kusini wanafikiri dunia ni sehemu mbaya

Zaidi ya asilimia 48 ya Vijana Afrika ya kusini wanaamini ya kuwa Dunia inazidi kuwa sehemu mbaya , huku asilimia 15% tu ndo wanafikiri inazidi kuwa sehemu nzuri. Katika uchunguzi huu asilimia 30% ya vijana wanaamini Afrika ya Kusini ni sehemu nzuri ya kuishi , huku asilimia 19% wakiamini ni sehemu mbaya kuishi.

Idadi kubwa ya vijana wa Afrika Kusini (68%) wanafikiri serikali yao inatumia nguvu ndogo sana kutatua mgogoro wa wakimbizi. Asilimia themanini na tatu (83%) ya vijana walisema ugaidi na siasa kali ndivyo vitu vinavyofanya wawe waoga kwa siku zijazo. uwiano sawa na asilimia 81% walikuwa na wasiwasi kuhusu uwezekano wa kutokea kwa migogoro na vita.

Utafiti pia unaonyesha kuwa vijana kwa ujumla wamekata tamaa kuhusu siku zijazo. Walisema fedha ni chanzo cha wao kuwa na wasiwasi huku asilimia (51%) kutaja masuala yanayohusiana na fedha  kama moja ya vyanzo vyawao kuwa na wasiwasi.

Hata hivyo, karibu asilimia (63%) ya vijana wanaamini kuwa ndoa za jinsia moja zipitishwe kisheria, ingawa wanawake wengi ndo walikubali kuliko wanaume (70% vs 54%).

Matokeo ya utafiti huu yalichapishwa na Varkey Foundation, kwa kuzingatia kwa kina maoni yaliyokusanwa na Populus.

Source: Sowetan Live

Soma na hizi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Close