Nyingine

Utafanya nini kama ingekuwa ni wewe?

Hii nimetumiwa kupitia whatsapp kuna jamaa anafanya kazi kwenye shirika moja linalojihushisha na masuala ya kusambaza vipodozi aliitwa ofisi kwa boss wake, akiwa anaelekea kwenye ofisi ya boss, secretary wake akampa barua.

Alipofika ofisi kwa boss wake boss akamwambia vitu vichache vinavyohusina na kazi kisha akamwambia afungue barua.

Haraka haraka jamaa akafungua barua na kuanza kuisoma ….kumbe ni barua ya kupandishwa cheo.

Boss akamwambia asome kwa sauti, jamaa akaanza kusoma kwa sauti, ghafla sura yake ikabadilika, pale alipoona tarehe ya sikukuu ya wajinga 1/4 mwisho wa barua.

Swali langu ni kama wewe ungekutana na tukio kama hili ungefanyaje?

SOMA NA HII:  80% watashindwa mchezo huu: ni Glass gani itajazwa kwanza?

Zinazohusiana

Toa Maoni Hapa:

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako