Habari za Teknolojia

Ushauri wa Obama kuhusu matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii

on

Aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama ameonya kuhusu matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii wakati wa mahojiano yasiyo ya kawaida tangu aondoke madarakani mwezi Januari.

mitandao ya kijamii

Obama alihojiwa na Prince Harry katika BBC Radio 4.

Alionya kuwa vitendo kama hivyo vinachanganya uelewa wa watu katika masuala magumu na kusambaza uvumi.

Mrithi wake Donald Trump ni mtumiaji mkubwa wa Twitter lakini Obama hakumtaja jina.

Obama alihojiwa na Prince Harry katika BBC Radio 4.

Obama alisema wale walio katika nyadhifa za uongozi wanastahili kuwa waangalifu wakati wanaandika katika mitandao.

Alielezea wasi wasi kuhusu siku za usoni ambapo ukweli utapotoshwa na watu watakuwa wakisema, watakuwa wakisoma na kusikiliza vitu ambavyo vitakuwa vikiridhisha maoni yao.

SOMA NA HII:  Ufahamu mto wa kulalia wenye uwezo wa kucheza muziki na kufatilia usingizi wako

Bw. Trump amelaumiwa kwa kutumia mtandao wa Twitter kupindukia licha ya yeye kusisitiza kuwa inamruhusu kuwasiliana moja kwa moja na watu wa Marekani.

About Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published.