Usalama Mtandaoni!! Kuingia na kutoka kwenye akaunti


Kuingia kwenye akaunti yako ya Google au akaunti zingine ni rahisi – huduma nyingi za mtandaoni siku hizi zimerahisisha jinsi unavyoweza kuingia kwenye akaunti yako.

Lakini wakati unatumia kompyuta zinazotumiwa na kila mtu kama kwenye mgahawabwake (internet cafe) au maktaba, kumbuka kwamba unaweza kuwa bado umeingia katika huduma zozote ulizokuwa ukitumia hata baada ya kufunga kivinjari. Hivyo, unapotumia kompyuta inayotumiwa na kila mtu, hakikisha umetoka kwenye akaunti yako kwa kubofya kwenye sehemu ya Ondoka (log out/sign out).

Ikiwa unatumia kompyuta zinazotumiwa na kila mtu mara kwa mara, tumia njia ya kuweka uthibitishaji wa akaunti yako kwa kutumia namba yako ya simu au swali maalum ili kuweka akaunti yako ikiwa salama, na uhakikishe umeondoka kwenye akaunti zako na kuzima kivinjari chako unapomaliza kutumia wavuti.

SOMA NA HII:  Nunua Simu za Tecno Mtandaoni kupitia ZoomTanzania & Jumia Online Stores

Kila siku Mediahuru tunakuleta mbinu mbalimbali za kujiweka salama na kuweka salama taarifa zako unapokuwa mtandaoni. Unaweza kusoma makala hii jinsi ya kubuni neno la siri thabiti na kuweka taarifa zako salama.

Endelea kutembelea mediahuru kila siku kupata elimu zaidi kuhusu masuala ya teknolojia, kumbuka kuandika maoni yako.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA