Usalama Mtandaoni!! Jinsi ya kuweka salama akaunti yako ya Gmail


Ikiwa unatumia Gmail, unaweza kufuata hatua hizi ili kuhakikisha akaunti yako ni salama.

Hakikisha barua pepe yako haisambazwi au kushirikiwa isipokuwa utake isambazwe au ishirikiwe

Angalia kitufe cha “Mipangilio ya Barua” katika Gmail ili uone mipangilio ya usambazaji na uwekaji kaumu inayowapa wengine idhini ya kufikia akaunti yako kuhakikisha barua pepe yako inaelekezwa sawasawa.

Ukisahau neno lako la siri , utahitaji njia ya kurejea kwenye akaunti yako

Google inaweza kukutumia barua pepe katika anwani ya barua pepe ya urejeshi ikiwa utahitaji kuweka neno la siri jipya, kwa hivyo hakikisha kuwa anwani ya barua pepe ya urejeshi imesasishwa na ni akaunti unayoweza kufikia. Pia unaweza kuongeza nambari ya simu kwenye wasifu wako wa Gmail ili upokee msimbo wa kuweka neno la siri jipya kupitia ujumbe wa maandishi.

Kuwa na nambari ya simu ya mkononi kwenye akaunti yako ni mojawapo ya njia rahisi na za kuaminika za kukusaidia kuweka akaunti yako salama. Kwa mfano, Google inaweza kutumia nambari ya simu kuwapa watu changamoto iwapo watajaribu kuvamia akaunti yako, na kukutumia msimbo wa kuthibitisha ili uweze kuingia kwenye akaunti yako iwapo hutakuwa na uwezo wa kuifikia. Kutoa nambari ya simu ya urejeshi kwa Google hakutakufanya usajiliwe kwenye orodha za mauzo au upigiwe simu nyingi na wanaofanya uuzaji kupitia simu.

Simu yako ya mkononi ni mbinu salama zaidi ya kuthibitisha utambulisho kuliko anwani yako ya barua pepe ya urejeshi au swali la usalama kwa sababu, tofauti na mbinu hizo zingine mbili, una umiliki halisi wa simu yako ya mkononi.

SOMA NA HII:  Mambo Yaliyompa Ushindi Mmiliki wa Facebook Dhidi ya Maseneta wa Marekani

Angalia ufikiaji au shughuli zisizo za kawaida kwenye akaunti yako

Kagua akaunti yako kila mara ili uone kama kuna shughuli usiyoifahamu au unayoitilia shaka. Bofya kwenye kiungo cha “maelezo” katika sehemu ya chini ya ukurasa ili upate anwani za IP zilizotumiwa hivi karibuni kufikia barua pepe yako, na maeneo yanayohusishwa. Ikiwa utaona shughuli unazozitilia shaka, badilisha nenosiri lako mara moja na uondoke kwenye akaunti yako. Pata maelezo zaidi kuhusu shughuli za kutiliwa shaka kwenye akaunti.

Wakati wa kuingia kwenye Gmail, unapaswa kuangalia ili uhakikishe anwani ya wavuti inaanza kwa https:// (na sio tu “http://”). Hii inaashiria kuwa muunganisho wako kwenye tovuti umethibitishwa na ni salama ni vigumu kuuchungulia au kuuchezea. Kwa vidokezo zaidi vya Gmail, angalia orodha ya usalama ya Gmail.

Ripoti unyanyasaji kutoka kwa mtumiaji wa huduma ya Gmail

Ukikumbana na mtumiaji wa huduma ya Gmail anayekiuka sera za Gmail, tafadhali kagua hatua zinazofuata zilizopendekezwa.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA