Sambaza:

Wakati wa Kampeni za uchaguzi, kamati ya kampeni ya Bwana Emmanuel Macron, ilivamiwa na makundi ya udukuzi ambayo yalichapisha habari muhimu za kundi lao katika mitandao ya kijamii, barua pepe sahihi ziliibiwa katika tarakilishi/kompyuta zao na kuchanganywa na zile bandia ili kuonyesha kuwa kamati hiyo ya Bwana Macron ni ya ubabaishaji tu.

Shirika la Upelelezi la Urusi lilijaribu kupeleleza kampeni ya uchaguzi wa Emmanuel Macron kupitia akaunti bandia za Facebook, kwa mujibu wa Reuters.

Ma-agent walionekana kama “marafiki wa marafiki” wa washirika wa Macron katika jaribio la kupata habari za kibinafsi kutoka kwao.

Urusi walitumia Facebook kujaribu kupeleleza kampeni ya urais wa Ufaransa - Ripoti

Wafanyakazi wa Facebook waliona shughuli hiyo katika mzunguko wa kwanza wa uchaguzi wa rais wa Ufaransa, baada ya kufatilia ilionekana ni zana inayotumiwa na “Russia GRU military intelligence unit” – inayojulikana kama Fancy Bear.

Facebook imethibitisha kwa Reuters kuwa iligundua jitihada hizo na kuamua kuzifunga akaunti hizo.

Reuters wamesema kuwa wakati wa kampeni, idadi ya akaunti za Facebook zilizofutwa nchini Ufaransa kwa sababu ya kukuza/kueneza propaganda au spam ilifikia 70,000 kutoka akaunti 30,000 zilizofungwa mwezi Aprili.

Microsoft pia imejitahidi kupambana na vita dhidi ya Fancy Bear, kuchukua hatua za kisheria dhidi ya “Internet domains” ambazo wapelelezi wa Kirusi walizisajili ambazo huonekana kama tovuti zinazohusiana na Microsoft.

SOMA NA HII:  Fahamu Maana ya Mtandao wa Intaneti na Faida Zake

Hii ilijumuisha anwani kama “netmicrosoft [.] Net” au “rsshotmail [.] Com”. Microsoft imefungua kesi ya kisheria ili kukamata domains yoyote ambayo wapelelezi wa kirusi wataisajili katika mtindo huu.

Orodha ya kikoa (domain) iliyotolewa ina domains 9,000, ikiwa ni pamoja na “infomicrosoftcenter [.] Com”, “win-newsmail [.] Com”, na “statistic-security-microsoft [.] Com”.

Ningependa kusikia kutoka kwako, je unafikiri kwa ongezeko la matukio ya uvamizi wa kimtandao serikali na vyombo vingine vya usalama vina nguvu ya kupambana na makundi haya ya udukuzi ? niandikie hapo chini sehemu ya comment.

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa Mediahuru Kila Siku Kwa Sababu Tunaaminika Katika Teknolojia.

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako