Urusi imesababisha mitandao ya kijamii kujitetea kwa Marekani


Wawakilishi wa mitandao mikubwa duniani ya Google, Facebook na Twitter wanatoa ushahidi mbele ya bunge la Seneta wa Marekani ili kuthibitisha kama Urusi ilitumia huduma zao kujaribu kujaribu kuingilia uchaguzi wa rais wa Marekani mwaka 2016.

kutoka kushoto muwakilishi wa Facebook Colin Stretch , Sean Edgett kutoka Twitter, na muwakilishi wa kampuni ya Google Richard Salgado wakitoa ushahidi wao mbele ya kamati ya bunge la seneti nchini Marekani

Makamu mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri wa Seneti, Mark Warner, aliwaambia waandishi habari alitarajia makampuni hayo kujieleza endapo huduma zao zilitumika vibaya.

Kampuni ya Facebook imeeleza mapema wiki hii kuwa Wamarekani milioni moja na ishirini na sita milioni wamegawanyika kufuatia maoni waliyotoa kuwa urusi inahusika .

Serikali ya Urusi imekanusha madai ya kujaribu kuingilia kati uchaguzi wa Marekani.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA