Upatikanaji wa intaneti: Vita ya makampuni ya teknolojia na serikali

Comment

Iwe ni kauli za chuki, propanganda au uanaharakati, serikali za ulimwengu zimeongeza jitihada za kubana maudhui yanayofikiriwa kuwa ni kinyume cha sheria katika mitandao ya kijamii.

Hapa nimekusogezea baadhi ya matukio yanayoonyesha jinsi nchi nyingine zinavyojaribu kuzuia ueneaji wa maudhui huku zingine zikijaribu kuwekea mipaka mitandao ya kijamii.

1. Sheria ya mitandao ya kijamii

Nchini Ujerumani waziri wa sheria Heiko Maas ametaka sheria itakayotoa faini kubwa kwa kampuni za mitandao ya kijamii kama Facebook, kwa kushindwa kuondoa taarifa zenye kauli za chuki. Lakini Facebook imepinga kwa kusema “kuzuia na kukabiliana na kauli hizo na habari bandia ni jukumu la jamii ambayo serikali haiwezi kuzuia”. Sheria hiyo hivi sasa inapitiwa upya na kamati ya bunge la Ujerumani.

2. Haki ya kusahauliwa

Mwaka 2014, mahakama ya Ulaya iliamua kwamba raia wa Ulaya wana haki ya kuomba mtandao wa kupata taarifa kama Google and Bing, na kuondoa matokeo ambayo si sahihi, si muhimu ama yaliyozidi kwa kile walichoomba. Ingawa Google ililalamikia hatua hiyo, ilifanya hivyo kwa ukaidi, na kuonya kwamba inaweza kufanya upatikanaji wa internet kuwa huru zaidi ulimwenguni.

3. Zuio la jumla.

Mnamo mwezi May, Ukraine iliweka vikwazo dhidi ya Jukwaa la mitandao ya kijamii la Urusi pamoja na huduma zake za tovuti. zuio hillo la jumla liliwaathiri mamilioni ya Waukraine, wengi wao walikuwa na wasiwasi kuhusu taarifa zao. Hatua hiyo iliwasukuma vijana kuandamana mitaani, wakiitaka serikali kurejesha uwezekano wa kuingia kwenye majukwaa kama VKontakte (VK), ambalo ni kubwa zaidi Urusi.

4. Usafirishwaji wa taarifa binafsi

Mwaka 2015, Mahakama ya Ulaya iliamua kwamba makubaliano ya miaka 15 ya “Safe Harbor” yaliyohusiana na usafirishwaji wa taarifa binafsi bila idhini ya kabla hayakuwa halali. Mwanafunzi wa sheria wa Kiaustria Max Schrems alianzisha mchakato wa kisheria dhidi ya Facebook kuhusiana na ufichuzi wa aliyekuwa mfanyakazi wa Usalama wa Taifa wa Marekani, NSA, Edward Snowden.

5. Kanuni

Nchini China, matumizi ya mitandao ya kijamii kwa kiasi kikubwa yanaendeshwa na serikali. China imezuia kabisa upatikanaji wa maelfu ya majukwaa na tovuti, ambayo ni pamoja na Facebook, Twitter, Instagram na Pinterest. Na badala yake China inawapa wananchi wake uwezo wa kufungua mitandao ya kijamii ya ndani kama Weibo na WeChat, ambayo inatembelewa na maelfu kwa mamilioni ya watumiaji kwa mwezi.

Chanzo: DW na Mitandao Mingine

Up Next

Related Posts

Discussion about this post

error: Content is protected !!