Sambaza:

Mwanamieleka maarufu , Mark Calaway anayefahamika zaidi kwa jina la  ‘The Undertaker’ amestaafu mchezo huu baada ya kuwa ndani ya ulingo kwa takribani miaka 30.  Baada ya kupigwa na Roman Reigns pale WrestleMania jumapili usiku, The undertaker mwenye miaka 52 alivua kofia yake maarufu , gloves na koti kisha akatoka ulingoni.


Taarifa mbalimbali zinasema, hatua hiyo ni njia ya jadi ya kumaanisha kustaafu miongoni mwa wana mieleka. Ingawa bado hakuna taarifa rasmi ya kustaafu, wachezaji wenzake wengi, nyota wa sasa na wa zamani katika mieleka, wametumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kuzungumzia swala hilo.

SOMA NA HII:  Nahitaji Antivirus, Je Wewe Unatumia Antivirus Gani Kwenye Kompyuta Yako?

Angalia video hapa chini:

Sambaza:

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako