Sambaza:

Unaweza kukaa muda gani bila kuwa na simu yako, kabla ya kuanza kuhangaika? Mfano uwe umeisahau mahali, imeisha chaji au labda umelazimishwa kuizima na kuiweka mbali?

Wanasaikolojia wamegundua kwamba jibu lake litakuwa dakika chache sana – hasa iwapo umri wako ni kati ya miaka 18 na 26.

Watafiti wanasema siku hizi watu wameanza kutumia simu kama mbadala badala ya kutangamana na watu. Wanalinganisha na jinsi mtoto anavyotulizwa hata kwa blanketi wazazi wake wanapokuwa mbali.

Utafiti huo ulianywa na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Eotvos Lorand nchini Hungary. Veronika Konok, mmoja wa watafiti, anasema: “Binadamu anaweza kuunga uhusiano mzito sana na vifaa, na vitu kama vile picha za watu muhimu kwake, au wanasesere.

SOMA NA HII:  Zifahamu ndege kubwa zaidi zilizowahi kuundwa duniani

“Simu ni muhimu sana kwa sababu bali na kuwa kifaa muhimu, pia ni hutusaidia kujumuika na wengine kupitia teknolojia.”

Veronika anasema anafikiri vijana wamekuwa na uhusiano mkubwa na simu zao.

“Watoto wanaotumia simu kuanzia utotoni, nafikiri uhusiano wao na simu utakuwa hata zaidi.”

Matokeo yake si ya kushangaza, kwani simu yako ikiishiwa na chaji au uipoteze kwa muda, mwenyewe unfahamu kwamba unaweza kutatizika si haba.

Wasiwasi wa kuwa mbali na simu yako umepewa jina – unaitwa nomophobia, ambao ni ufupisho wa “no-mobile-phone phobia”.

Tatizo hilo huathiri vijana wanne kati ya watano kwa mujibu wa baadhi ya utafiti.

Je kwa upande wako unaweza kukaa muda gani bila kuwa na simu yako? Tuambie kupitia sehemu yetu ya maoni.

Toa maoni yako.

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako