IntanetiMaujanja

Je unaelewa utofauti kati ya Website, Domain Name na Hosting ?

Ni rahisi kuchanganyikiwa na misamiati ya ulimwengu wa Website, Kama ndio unaanza basi leo tunaelezea vitu vitatu muhimu kuhusu website ambavyo ni website, domain name na hosting.  Katika makala hii, tutajadili tofauti zote kati ya vitu hivyo kwa lugha rahisi.

Ingawa si lazima ujue misamiati yote ya Website na Website Design, ila ni vyema ukawa na uelewa wa baadhi yake. Habari njema ni kuwa, Mediahuru tunakuletea makala mbalimbali zitakazokujengea ufahamu wa masuala ya Website.

Domain names, websites na web hosting ni huduma tatu zinazounganishwa pamoja ili kutoa huduma ya mtandaoni lakini ni tofauti sana kulingana na ufanyaji kazi wake.

Website ni nini

Website ni mjumuiko wa mafaili kwenye mtandao (World wide Web) , kwa wengi wanavyoujua kama Internet. Chukulia mfano wa vitabu kwenye shelfu. Vile vitabu ndiyo vinaitwa Website, kwani kwenye kila kitabu kutakuwa na taarifa nyingi nyingi kwa kila kurasa (Hii inafananishwa na kurasa za Website, Web Pages). Ili uweze kuwa na Website iliyokamilika, lazima uwe na vitu vingine kama Web Hosting na Domain Name, hii ni sawa na Shelfu la vitabu na jina la kitabu.

Kwenye Website, taarifa huandikwa na lugha nyingi za Web, mara nyingi lugha zinazotumika ni kama HTML, CSS na Javascript. Lugha hizi hutoa maelekezo kwa browser (Google Chrome, Mozila Firefox, Internet Explorer nk) ni jinsi gani hiyo Website ionekane na ifanyeje kazi. Muandishi atatumia lugha hizo kuwakilisha vitu tofauti, kama ilivyo kwenye vitabu tunavyotumia. mwandishi wa kitabu cha Ngoswe ni tofauti wa kile cha Kuli.

SOMA NA HII:  Mambo 5 Usiyoyajua Kuhusu Mtandao wa Instagram

Domain Name

Watu wengi wamekuwa wakichanganya Domain Name na Website, hivi ni vitu viwili tofauti. Ili mtu aweze kufungua Website yako, anahitajika kuandika jina la Website kwenye browser (Domain Name). Hapo awali kabla ya matumizi ya Domain Name kuanza, hakukuwa na majina ya Website, bali watu walitumia namba za utambulishi wa kifaa kwenye Internet (IP), mfano ukitaka kufungua website ya mediahuru.com ulitakiwa uandike 123.456.789.101. Sasa, baada ya kuona ni ngumu kukariri hizi namba ndipo walipoamua kuja na majina ya Website.

Kwa kawaida, huwa ina sehemu mbili, sehemu ya kwanzani TLD na sehemu ya pili ni Jina halisi, TLD (Top Level Domain) ni kama .co.tz, .com, .or.tz nk, wakati jina lenyewe ni kama Mediahuru, DealVictory nk, hivyo ukichanganya ndiyo unapata mediahuru.com dealvictory.co.tz nk kutegemeana umechangua TLD ipi. Hiz TLD hutofautiana kulingana na matumizi na pia wapi zimetolewa. Unaweza kupata maarifa zaidi ya Domain kwenye hii makala Vitu 10 vya Kuzingatia unapochagua majina ya website

Web Hosting

Website Hosting ni kama vile nafasi uliyokodi kwa ajili ya biashara. Mfano unapokodisha nafasi mara nyingi unakuta hakuna kitu, hakuna shelfu wala viti. Ni sawa na Hosting, unaponunua Website Hosting usitegemee kuwa tayari ina Website iliyokamilika. Utahitajika ama utengeneze mwenyewe ama ukubaliane na aliyekuuzia nafasi akutengenezee, sawasawa na maisha ya nje ya Website.

SOMA NA HII:  Je natakiwa kumiliki website au blog ?

Bila Website Hosting, hakuna kitakachoendelea na hautoweza kufanya lolote kwakuwa mafaili yako hayatokuwa na sehemu ya kukaa na watu waweze kuyaona.

Domain Name vs Website vs Web Hosting

Kwa maelezo ya juu, utaona kuwa, Website, Domain Name na Website Hosting ni vitu vinayoshirikiana. Unavihitaji vyote ili Website yakoiwe hewani na kuonekana na watu wote Tanzania na Dunia kwa ujumla (Internet). Domain Name litaiita Website ambayo ina makazi kwenye Website Hosting. Na pale mtu anapobonyeza www.mediahuru.com basi mafaili yaliyo kwenye Website yatafunguliwa kulingana na jinsi ilivyotengenezwa.

Ukiwa na swali lolote kuhusu Website Design, Website Hosting na Domain Name Registration usisite kuwasiliana nasi.

Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako