UltraSharp monitor mpya ktoka Dell ni “38-inch curved WQHD monitor”


Ingawa siku za karibuni “ultrawide monitors” za aina mbalimbali zimeingia soko, lakini Dell imekuwa mfalme kwa kushika nafasi ya kwanza (ikifuatiwa kwa karibu na LG) . Sasa kampuni ya Dell imerudi tena kwa kuzindua monitor ya ajabu, “38-inch curved ultrawide monitor”, na mimi naitamani vibaya sana.

Monitors za Dell UltraSharp zinapewa sifa kubwa na wataalamu mbalimbali (ni nzuri kwa sababu – zina mvuto wa ajabu). Uzinduzi wa bidhaa mpya kwenye familia hii unaleta utawala wa haki kwenye kizazi cha teknolojia.

Dell UltraSharp 38 Curved Monitor (U3818DW) ni 37.5-inch ultrawide curved screen monitor ya kwanza kutoka kwa kampuni hiyo. Dell wanasema kwenye kuonyesha maudhui mbalimbali ina uwezo asilimia 25 zaidi ya  34-inch WQHD 21: 9 monitor.

Dell UltraSharp 38 Curved Monitor (U3818DW) zinajibu swali la kila aina kuhusu monitor unayohitaji ukubwa wake unaleta tija kwenye uzalishaji. Ina “3440 x 1440 resolution, 100w USB-C connection” inayoweza kuchaji laptop yako huku ikisafirisha taarifa.

Upande wa pili bei yake inakadiliwa kuwa takribani shilingi 3354800. Unaweza kununua Dell UltraSharp 38 Curved Monitor kwenye mtandao wa Dell.com kwanzia tarehe 23 Juni.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA