Habari za Teknolojia

Ukosefu wa Ajira Wasababisha Website ya Chuo Tanzania Kudukuliwa

Kumekuwa na matukio ya kuvamiwa kwa tovuti za taasisi mbalimbali na watu ambao wanasema wanataka ajira. Ikiwa ni muendelezo wa udukuzi nimekutana na ujumbe kwamba tovuti ya TIIS (Training Institution Information System) imedukuliwa, Watu waliofanya udukuzi wameweka ujumbe kwamba wanataka ajira.

Tembelea tovuti ya www.tiis.go.tz ushuhudie mwenyewe:

Sio mara ya kwanza kwa tovuti za taasisi mbalimbali hapa nchini kuvamiwa na wadukuzi kwani tovuti ya TASAF imedukuliwa toka tarehe 21 November, pitia hapa TASAF hAcKeD.

Na pia Mnamo tarehe 30 October tovuti ya vyuo vikuu TCU ilidukuliwa pamoja na sub domain ya faas.tcu.go.tz na pms.tcu.go.tz sasa zimefanyiwa marekebisho.

Je ni sahihi kwa hackers kutumia njia hii kutoa malalamiko yao? Unazungumziaje uwezo wa wasimamizi wa tovuti za serikali katika kusimamia usalama?

SOMA NA HII:  Utaalamu mpya wa kukuza yai la Mwanamke katika maabara umegunduliwa
Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako