Nyingine

Ujumbe wa Nikki Mbishi kuhusu wanaomkosoa Songa.

Nikki mbishi ni moja kati ya wasanii wa hiphop wenye misimamo katika mambo mengi. Kwa sasa anatamba na wimbo wake wa “Dada pumzisha mwili wako” ambao ameachia hivi karibuni.

Mapema leo kupitia mtandao wa Instagram Nikki Mbishi ameandika ujumbe wake kwa wote ambao wanamkosoa Songa baada ya kutoa wimbo wake wa Double tap.

Nikki Mbishi ameandika “Hahahaha anayemsema Songa yeye ana njia yake ya kuingiza kipato hawazi Songa hasomi hana ajira na umri unakwenda na majukumu hayampungui na zile oi oi zenu za mdomoni zinazidiwa na mawaki sasa sijui waki ni nani? Kama harakati ni ukombozi mbona harakati hazimkomboi Songa?
Harakati ni kutoka kwenye utumwa wa fikra,uchumi na mwelekeo bora wa kimaisha,kwani ni nani kati yenu hajivunii kuwa na makazi,mavazi,lishe bora na anasa zote za maisha kama miradi ya biashara kubwa,hisa,maisha
bora ya kisasa kulingana na wakati bila kusahau kurudisha fadhila isiyorudishika kwa wazazi wako na jamii yako yote yaani wafuasi na mashabiki.
Songa kufanya muziki atakavyo hakumfanyi awe amepungua uwezo wake wa kuandika,kutunga na kurap na kama huamini njoo na emcee/rapper wako utaamini nisemayo kwa maana UWEZO au KIPAJI ni KARAMA na sio kwa kila MTU. Nukuu ya leo: “HARAKATI KWA MAISHA BORA”

Sio kuchoma CD ya Soga Za Mzawa ya miaka mitano iliyopita kisa wimbo wa leo. #ShabikiAndazi

Soma na hizi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Close