Ufahamu mto wa kulalia wenye uwezo wa kucheza muziki na kufatilia usingizi wako


Sasa ni 2018, na nimuda wa mito yetu ya kulalia kuongezewa teknolojia mpya. Rem-Fit’s Zeeq pillow imekuja na vitu vizuri sana, pengine uwezo wa kuboresha usingizi wa mtu, kwa njia mbalimbali. Wengine wanapenda muziki wakati wa kulalala wakati wengine wanahitaji msaada kupunguza kukoroma na kufanya uchambuzi wa mfumo wa usingizi.

Mto unakuja katika matoleo matatu tofauti. Snore pillow yenye mfumo wa vibration ambao polepole unaweza kufanya mtu abadilishe jinsi alivyolala kwa  lengo la kupunguza kukoroma. Tunes pillow ina uwezo wa kucheza muziki kutoka kwenye simu janja iliyounganishwa kupitia spika nane zilizowekwa kwenye mto huo. Kampuni hiyo imesema mtu aliyelalia mto huu tu ndio atakaye sikia muziki huo. Pia kuna tracker pillow ambayo inafungua sensors na inatumia analytics kumpa taarifa mtu aliyelala kuhusu mfumo wake wa kulala na kutoa mapendekezo ya jinsi ya kufanya usingizi uwe bora zaidi.

SOMA NA HII:  Jinsi Unavyoweza kutumia WhatsApp kwenye Kompyuta yako

Kampuni hiyo kutoka Chicago-nchini Marekani inaonyesha imefikilia mbali zaidi kuhusu vipengele vya mto huu. Kwenye mto huu wa kulalia pia unaweza kupanga unataka muziki ucheze kwa muda gani. Pia kuna mfumo wa alarm ndani ya mto ambao utasaidia kumwamsha mtu aliyelala. Mto pia unafanya kazi na IFTTT, Alexa na Google HealthKit katika njia mbalimbali.

Kitu pekee ambacho naona hakijakaa sawa kwenye mto huu ni kuwa mto huu wa kulalia unatakiwa kuchajiwa kila baada ya wiki mbili. Mto pia unatakiwa kuunganishwa na mtandao wa Wifi , kitu ambacho sikudhani kama kinaweza kuwa na umuhimu

SOMA NA HII:  Kenya yatengeneza satelaiti yake kurushwa anga za juu Machi mwaka huu

Mto huu wa kulalia unapatikana hapa kwa gharama ya $200 kwa sasa.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA