Nyingine

UEFA yaamua kubadili utaratibu wa kupiga mikwaju ya Penalti

Shirikisho la Soka barani Ulaya UEFA limesema linatathmini utaratibu wa kupigwa kwa mikwaju ya penalti baada ya mechi na kuufanya uwe wa haki zaidi. Shirikisho hilo tayari limeanza kufanyia majaribio utaratibu mpya.

Chelsea walishindwa na Manchester United fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2008 wakipiga penalti wakiwa wa pili

Badala ya klabu kubadilishana mmoja baada ya mwingine, UEFA inatafakari uwezekano wa kufuata utaratibu sawa na unaofuatwa katika mchezo wa tenisi.

Utaratibu huo unafanyiwa majaribio katika michuano ya ubingwa wa Ulaya kwa wachezaji wa chini ya miaka 17 ambayo ilianza Croatia Jumatano.

Utaratibu mpya unaitwa ABBA ambapo mchezaji wa timu A akianza, atafuatwa na wawili wa B kabla ya mchezaji wa A kupiga tena. Sarafu bado itarushwa kuamua atakayeanza.

Pendekezo hilo linatokana na ugunduzi kwamba timu inayofuata kwa kupiga penalti wachezaji wake hukabiliwa na shinikizo zaidi, kwani kila mara huwafuata wapinzani.

Utafiti unaonesha kwenye matuta, klabu inayotangulia kupiga mkwaju imekuwa ikishindwa katika asilimia 60 ya michuano yote.

Mfumo huo umependekezwa na IFAB ambacho ni chombo pekee chenye mamlaka ya kubadili sheria za soka.

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *