Udukuzi wa mitandao waendelea kuyakumba Makampuni mengi duniani

Makampuni kote duniani yanaripoti kuwa yamekumbwa na udukuzi mkubwa wa mitandao. Kampuni ya matangazo ya biashara ya Uingereza WPP ni kati ya makampuni yanayoripoti matatizo hayo.

Makampuni nchini Ukrain ikiwemo ya kusambaza umeme ya serikali na uwanja wa ndege mjini Kiev yalikuwa miongoni mwa yale ya kwanza kuripoti matatizo hayo.

Baadhi ya wataalamu wanasema kuwa huenda ukawa ni udukuzi wa kuomba fidia sawa na ule wa mwezi uliopita wa Wannacry.

Alan Woodward ambaye ni mtaalamu wa komputa katika chuo cha Surrey, anasema kuwa hicho kinaonekana kuwa sehemu ya kirusi kilichoibuka mwaka uliopita.

Baadhi ya mashirika yanayoripoti tatizo hilo ni pamoja na Benki kuu nchini Ukrain, na kampuni ya kuunda ndege ya Antonov na mashirika mawili ya posta.

Kampuni ya mafuta nchini Urusi ya Rosneft na ile ya Denmark ya Maersk, pia nayo yanakumbwa na matatizo zikiwemo ofisi zake nchini Uingereza na Ireland.

SOMA NA HII:  Twitter sasa ina watumiaji milioni 330 kila mwezi

COMMENTS

WORDPRESS: 0