Sambaza:

Infinix Hot 5 ni toleo la tano kutoka katika mfululizo wa simu za Hot ambazo ni smartphones za bei nafuu. Kifaa hiki kina betri yenye nguvu, fingerprint scanner na inatumia mfumo endeshi wa Android 7.0 (Nougat).

Infinix Hot 5 imetoka baada ya Infinix Hot 4 iliyozinduliwa mwaka 2016. Nilifurahishwa sana na Hot 4 hasa ukilinganisha ubora wake na bei , na natumaini Hot 5 inaishi kwenye dunia hiyo.

Hapa chini ni maelezo maalum ya Infinix Hot 5 unapaswa kuangalia ikiwa upo kwenye soko la kutafuta smartphone mpya.

Sifa kamili za Infinix Hot 5 ni kama ifuatavyo:

Kama unavyoona kwenye sifa za Infinix hapo juu, Infinix Hot 5 ni simu janja ya bei ya kawaida. Sifa zake hazishangazi lakini zinakubalika kwa smartphone ambayo itakuwa sokoni kwa bei ya chini ya Tsh 250,000.

Kamera zake zina ubora wa kutosha kwa watumiaji wengi, isipokuwa wale ambao wanapenda kupiga picha kupitiliza. Kwa uhifadhi wa vitu, kuna nafasi ya GB 16. Pia unaweza kuweka mpaka memori ya ukubwa wa GB 128.

Je, utanunua Infinix Hot 5 itakapo zinduliwa nchini Tanzania ? Je! Ina thamani ya pesa yako?

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako