AndroidSimu za MkononiUchambuzi

Uchambuzi : Ifahamu Tecno Camon C8, Bei na Uwezo Wake!

Tecno Camon C8 (a.k.a Tecno Camon8) ni smartphone ya Androidyenye bei nafuu  imetengenezwa ili kuwapa watumiaji uwezo wa kupiga picha bora na ina uwezo wa kushangaza wa kasi ya data. Inajumuisha prosesa ya quad-core, kamera yenye nguvu na betri kubwa, huku ikiwa na kioo kikubwa na programu endeshi ya Android (Lollipop).C8 imeboreshwa katika Tecno Camon C9 na Tecno Camon CX.

Sifa kuu na uwezo wa Tecno Camon C8

  • Kioo: Ukubwa wa inchi 5.5, ubora wa kioo ukiwa 720 x 1280 pixels
  • Uwezo: 1.3GHz quad-core Processor na RAM ya 1GB
  • Mfumo wa uendeshaji: Android 5.0 (Lollipop)
  • Uhifadhi: 16GB ya uhifadhi wa ndani pia unaweza kuweka memori hadi 32GB
  • Kamera: Kamera ya nyuma ina 13MP na kamera ya mbele ni 5MP
  • Teknolojia nyinginezo: 3G Data
  • Laini za simu: Inakubali laini 2
  • Betri: 3000 mAh ina uwezo wa kuchaji kwa haraka

Ubora na Kioo

Simu hii ina muundo wa kupendeza na wa kifahari, lakini haimaanishi itashinda tuzo kwa muonekana wake. Bado haijulikani jinsi ilivyo nyembamba . Tecno Camon C8 ina kioo chenye kubwa wa inchi 5.5 kina uwezo wa HD. Ubora wa kioo, umeunganishwa na teknolojia ya IPS, inamaanisha kuwa utafurahia zaidi muonekano wa vitu mbalimbali kwenye simu hii.

Kamera na Uhifadhi

Tecno Camon C8 inaonekana imeundwa kwajili ya wapenzi wa kupiga picha ikiwa na kamera ya nyuma yenye megapixel 13 na kamera ya selfie ya megapixel 5. Chakushangaza, Tecno Mobile imeweka LED flash mbili na autofocus kwenye kamera kuu.

SOMA NA HII:  Ifahamu simu ya Google Pixel 2 bei na Sifa zake

Inasema kamera zote zimeundwa ili kuwawezesha watumiaji kuchukua picha nzuri hata katika mazingira ya mwanga. Hifadhi ya kutosha ya GB 16 inapatikana kwenye smartphone hii, na inaweza kupanuliwa hadi kufikia 32 GB kupitia slot ya microSD.

Prosesa, RAM na Sifa Zingine

Tecno Camon C8 inakuja na prosesa ya ‘quad-core’ yenye kiwango cha 1.3 GHz hii ikiwa na pamoja na RAM ya GB 1. RAM GB 1 ni kiwango kinachotosha tu katika kuhakikisha simu yako inaweza kufanya kazi vizuri ata pale ambapo kuna apps kadhaa zinafanya kazi kwa wakati mmoja.

Tecno Camon C8 inatumia Android 5.0 Lollipop – toleo zuri la programu endeshaji ya Android. Simu nyingi za Tecno zinatumia toleo la Android 4 na hivyo Tecno Camon C8 imekuwa moja ya simu mpya kabisa katika utumiaji wa toleo la Android Lollipop.

Betri lenye kiwango kizuri tuu cha chaji, nacho ni mAh 3000, kwa kiwango hichi basi utegemee si chini ya siku nzima ya bila kuchaji katika matumizi ya kawaida.

Tecno Camon C8 inapatikana kwa takribani Tsh 300,000/=, kutegemea na eneo uliopo basi bei inaweza ikawa chini au juu kidogo ya hapo.

Je ushatumia au kuijaribu Tecno Camon C8? Je unadhani ni simu unayoweza kufikiria kununua kama hela unao ? Tungependa kusikia kutoka kwako.

Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako