Habari za Teknolojia

Twitter sasa ina watumiaji milioni 330 kila mwezi

on

Moja ya mtandao mkubwa zaidi wa kijamii, Twitter sasa una watumiaji kazi (active users) milioni 330, na kuongeza watumiaji milioni 4 wa kila mwezi kwa robo ya mwaka, kutoka milioni 326 kwa robo ya kwanza ya mwaka na milioni 317 wakati huu mwaka jana.

watumiaji-mediahuru

Ingawa haya sio maboresho makubwa kwa ujumla, kuongeza kwa idadi ya watumiaji ni moja ya mambo makuu ambayo Twitter na wawekezaji wake wamekuwa wakiyatafuta.

Watumiaji wa kila siku pia wanaongezeka kwa asilimia 14 kwa kila mwaka, ingawa Twitter haikutoa takwimu halisi juu ya idadi yake kwa ujumla.

SOMA NA HII:  Ripoti : Idadi ya watumiaji wa Intaneti yaongezeka Kufikia milioni 23

Hata hivyo, Twitter ilisema kuwa imekuwa ikipoteza watumiaji wa kila mwezi tangu mwishoni mwa mwaka 2014, kupungua kwa watumiaji kwa robo mbili za mwaka kati ya milioni 1 hadi 2. Takwimu zilizobadilika zina maana kwamba kampuni ilipoteza watumiaji wakati wa majira ya joto, badala ya kukaa kwenye mkondo wake wa kuongezeka kwa watumiaji kila siku.

Mapato yaliyoripotiwa ya Twitter ya dola 590,000,000, ni chini ya $ 616 milioni wakati huu mwaka jana, sawa na  kushuka kwa asilimia nne. Bado, hasara ya kampuni hiyo imepungua, kwa kupata hasara ya dola milioni 21, chini ya $ 103 milioni wakati huu mwaka jana.

Nambari za Twitter zinazidi kushangaza watu kwa kuwa chini ikilinganishwa na mitandao mingine ya kijamii – hasa inayomilikiwa na Facebook.

Instagram ina watumiaji milioni 800 kila mwezi, baada ya kuongeza milioni 200 ambayo ni kidogo zaidi kuliko mwaka uliopita. WhatsApp na Facebook Messenger zina watumiaji zaidi ya bilioni 1 kila mwezi, na Facebook yenyewe ina zaidi ya bilioni 2. Snapchat, ambayo imejikuta kwenye ukuaji wa polepole, inaonyesha tu watumiaji wa kila siku, lakini ni karibu nusu ya watumiaji wa Twitter kila mwezi, ikiwa na watu milioni 173 wanaotumia programu hiyo kila siku.

About Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published.