IntanetiTwitter

Twitter inajaribu Lite Android app

Twitter inajaribu programu ya Android ambapo ipo sawa na tovuti yake ya Lite, kampuni hiyo iliiambia TechCrunch.

App hiyo inajaribiwa katika nchi ya Ufilipino, na inalenga watumiaji ambao hawawezi kufikia mitandao ya LTE au ambao wana simu za mkononi zenye uhifadhi mdogo.

Vipengele vikuu vya Twitter zimo kwenye app, lakini hupunguza “data-intensive media” – na inajumuisha hali ya “Saver Data” inayofanya picha zisionekane.

Twitter walisema hii inaweza kuokoa hadi 70% kwenye matumizi ya data ikilinganishwa na programu/app ya kawaida.

Lite app bado iko katika majaribio, na Twitter haijasema iwapo itatolewa duniani kote.

SOMA NA HII:  Google Assistant Sasa ina Chaguo la Sauti ya Kiume. Jifunze Jinsi ya Kuwezesha.

Zinazohusiana

Toa Maoni Hapa:

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako