Tweet ya Kylie Jenner yashusha mapato ya mtandao wa Snapchat


Mwanadada Kylie Jenner kutoka Familia ya Kardashin amekuwa mmoja ya watu waliopaza sauti zao kuukosoa mtandao wa kijamii wa Snapchat.


Kylie ameukusoa mtandao huo hapo jana kupitia mtandao wa Twitter kutokana na mfumo wake uliopo kwa sasa kwani unasadikika kuwa mgumu na kufanya watu washindwe kuutumia vyema kama hapo awali.

Mtandao wa Snapchat umekuwa ukiongezeka watumia kila siku hata hivyo mapema wiki hii mwanzilishi wa mtandao huo aliweka bayana hali ilivyo katika mtandao huo.

Kufuatia ukosoaji huo wa Kylie ambaye ana watu milioni kadhaa wamamfuatilia kumeweza kupelekea hisa za mtandao wa Snapchat kushuka kwa asilimia 6.1% sawa na thamani ya dola bilioni 1.3.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA