Nyingine

TWAWEZA: Kiingereza bado tatizo, 52% ya darasa la 7 hawawezi kusoma hadithi ya darasa la 2

Taasisi Twaweza wamezindua ripoti ya Tathmini ya 6 ya matokeo ya kujifunza nchini ya #Uwezo huko Dodoma. Tathmini hiyo imebainisha matokeo ya kujifunza pamoja na mazingira ya kujifunzia nchini Tanzania kutokana na utafiti ya mwaka 2015.

Katika moja ya matokeo ni kuhusu uwezo wa kusoma kiingereza katika Shule za Msingi. Uwezo huu umepimwa kwa darasa la 3 na la 7 kwa kutumia mtaala wa darasa la 2 kwa wanafunzi wote.

13% (Mmoja kati ya Kumi) tu ya wanafunzi wa darasa la 3 waliweza kusoma hadithi ya kiingereza ya darasa la 2. Kama tu hiyo haitoshi 52% ya Darasa la 7 walishindwa kusoma hadithi ya kiingereza ya Darasa la 2.

Je Matokeo haya yanaashiria nini? Je ni ubovu wa mitaala ya kiingereza? Je ni ugumu wa lugha hii?

SOMA NA HII:  Kuwa mkweli! Jina gani umetumia ku-save namba ya simu ya mama yako?

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published.