TV Zina Madhara Makubwa Kiafya Katika Vyumba Vya Kulala Watoto


Utafiti uliofanyika katika chuo cha wanasayansi cha London umegundua kuwa watoto wenye TV katika vyumba vyao vya kulala wana uwezekano mkubwa wa kuwa na uzito wa kupindukia kuliko wale ambao hawana,

Watafiti walibaini kuwa watoto wasichana kadri wanavyokaa muda mrefu wakitazama TV, ndivyo wanavyokuwa na uwezekano mkubwa wa uzito wao wa mwili kuongezeka. Watafiti wanasema kuna haja ya haraka sasa ya kuchunguza uwezekano huo kwa watumiaji wa vipakatanishi (laptops) na simu za mkononi (mobiles).

Utafiti huo uliochapishwa katika Jarida la Kimataifa kuhusu Unene wa kupindukia (International Journal of Obesity) ulitathmini data kutoka kwa watoto wadogo zaidi ya 12,000 nchini Uingereza pia umegundua watoto wanapotumia muda mefu kutazama TV hupata madhara mengi ya kiafya.

Wanasayansi hao walibaini kuwa zaidi ya nusu ya watoto waliokuwa na TV katika vyumba vyao vya kulala wakiwa na umri wa miaka saba. Wazazi waliulizwa kueleza ni kwa kiwango cha saa ngapi kwa siku watoto wao hutazama TV kwa ujumla .

Watafiti wanajiuliza ikiwa matumizi ya simu za mkononi (mobiles) pia yana uhusiano na kuongezeka kwa unene wa mwili wa kupindukia

Baadae , watoto hao walipofikia umri wa miaka 11, watafiti walipima viwango vya uzito wao wa mwili kulingana na kimo chao cha urefu kwa kuangalia asilimia ya mafuta ya mwili waliyonayo.

Wasichana waliokuwa na TV ndani ya vyumba vyao vya kulala wakiwa na umri wa miaka saba walipatikana na asilimia 30% ya uwezekano wa kuwa na uzito wa mwili wa kupindukia wanapofika umri wa miaka 11, wakilinganishwa na watoto wenzao ambao hawakuwa na TV vyumbani mwao.

Kwa wavulana, hatari hiyo iliongezeka kwa asilimia 20%.

Mtafiti Dr Anja Heilmann, alisema:

“utafiti wetu unaonyesha kuwa kwamba kuna ushahidi wa wazi wa uhusiano baina ya kuwana TV chumbani kwa mtoto na kuongezeka kwa uzito wa mwili kwa mtoto miaka michache baadae.”

Watafiti wanasema hawawezi kuwa na uhakika juu ya nini kinachosababisha uhusiano baina ya kutazama TV na kuongezeka kwa mwili, lakini wanasema huenda sababu ikawa ni watoto wenye TV vyumbani kusinzia kwa muda mfupi wakitumia muda mrefu kuitazama katika vyumba vyao vya kulala ama ulaji wa kiholela wanapotazama TV.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA