Tumia camera kupiga selfie, unapata majibu ya saratani


Wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Washington, Marekani wamegundua njia mpya ya kupima saratani ya kongosho na magonjwa mengine kwa kutumia App iliyopewa jina la BiliScreen ambapo mgonjwa atakuwa anapiga picha za mbele ya camera ‘SELFIE’.

App ni maalumu na inatumiwa kwenye mfumo wa simu za smartphones zenye camera, computer au vifaa vya umeme vyenye uwezo wa kupiga picha ambapo kwa mtu kupiga selfie camera inaweza kugundua na kuweka wazi dalili zozote za magonjwa hayo zilizopo katika mwili wake.

App hii imetengenezwa kwa lengo la kusaidia upimaji wa dalili za saratani ya kongosho ambazo kwa kawaida huwa hazionekani zikiwa katika hatua ndogo badala yake huanza kuonekana pale tu uvimbe unapokuwa mkubwa na kutapakaa mwilini, hivyo kushindwa kuizuia mapema.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA