Sambaza:

Mziki wa Hip hop, Rap na Bongofleva ulianza kunajisiwa around 2004 na kupoteza kabisa ladha ya ubunifu, vionjo, burudani na elimu kwa jamii. Aidha wapo waimbaji wa enzi hizo na wapo watayarishaji wa muziki (Producers) ambao ndio wameufikisha hapa muziki wetu.

Wafuatao ni watayarishaji mahiri wa muziki waliopata kutokea Bongo hii;

P. FUNK MAJANI – BONGO RECORDS

Paul Matthysse ( P Funk ) ni mtayarishaji wa muziki na pia mmiliki wa Studio ya Bongo Records iliyopo jijini Dar es Salaam, Tanzania.

P Funk a.k.a. Majani, ni nusu Mtanzania na nusu Mdachi. Kwenye miaka 1991-92 wakati yupo bado shule IST (International School Of Tanganyika. Alikuwa mtundu mtundu kwenye studio za shule.. kupiga- piga midundo mbali mbali ya hapa na pale na kufoka-foka (Rap music) na pia alikuwa mbele sana kwa kupiga musiki kwenye Pati mbali mbali.

P-Funk alienda kusoma Mlio (sound) engineering kwa miezi 18 pale Amsterdam, Netherland kabla ajaingia kwenye kutayarisha muziki. Mwaka 1995 akiwa na vifaa vyake vichache alianzisha kampuni yake ya kurekodi muziki nyumbani kwake. Na ni katika kipindi hicho hicho neno ’Bongo’ lilipokuwa linatawala katika misemo ya kiswahili cha mitaani na lilikuwa linaelezea hali halisi ya maisha ya Dar es Salaam na ndio kipindi hicho album ya Bongo ilipozinduliwa.

Majani pia amewahi kupata tuzo ya Kili Music Awards mara tatu, mwaka 2003, 2005 na 2006. Kwanza alianza kwa kumpandisha chati Juma Nature, akaendelea kwa kutayarisha santuri ya Solo Thang, AY, Zay B, Sista P, Mike T, Afande Sele, ,  Jay Mo, Ngwair(R.I.P) na pia alishawahi kufanya kazi na Professor Jay alipotoa santuri yake mwenyewe.

P Funk ametengeneza nyimbo kama Mvua na jua ya Jay Mo, Anakuja ya Sister P,  Nini mnataka ya Pig Black, Hayakuhusu ya Rah P,  Kigetogeto ya Juma Nature na nyingine kibao.

SOMA NA HII:  Je una bashiri "kubeti" ili kujikwamua na matatizo ya kimaisha ?

 

MASTER JAY- MJ RECORD

Joachim Kimario (Master Jay) ni muandaaji wa muziki nchini Tanzania Master Jay alizaliwa Tar. 8 Agosti mwaka 1973 akiwa mtoto pili katika familia ya marehemu Mzee Sylvan Kimario na mama yake Scholastica Kimario.

Master pia amewahi kupata tuzo ya Kili Music Awards mara mbili, mwaka 2004 na 2007.  Master Jay ana uwezo mkubwa sana wa utengenezaji wa muziki hasa kufanya mixing kali za muziki.

Master Jay alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi Upanga lakini aliishia darasa la tano na kuhamishiwa Botswana baada ya familia yake kuhamishiwa nchini huko kikazi.

Ilivyofika mwaka 1989 alipata digrii ya electronics katika chuo kimoja kilichopo bara la Ulaya mbali na shughuli za kimuziki.

Mnamo mwaka 1996 Master Jay aliamua kujishulisha kabisa na maswala ya Utengezaji wa muziki kwa kuamua kuanzisha rasmi studio yake aliyoipa jina lake la “Mj Production” japo kuwa babake alikuwa haja ridhia hilo. Baadae akatoa wimbo wa kundi la Kwanza Unit na baada ya muda kidogo tena akatoa nyimbo ya kundi la 4 Crews Flavour, baada ya hapo ndipo mzee wake alipoanza kuoynesha moyo na kuanza kukubali Anachofanya na hii ilimpa moyo wa kufanya kazi kwa bidii zaidi.

Aliweza kuibua vipaji vikubwa ambavyo vilifanya vizuri katika medani ya muziki wa Tanzania kama vile Lady Jay Dee , Mike T Mnyalu bila kusahau Kundi la Kwanza Unit na wengineo.

MIKA MWAMBA- FM STUDIO

Miikka Aleksanteri Kari (amezaliwa tar. 16 Oktoba 1971, mjini Helsinki, Finland) ni mtayarishaji wa muziki na mhandisi wa sauti toka nchini Finland-Tanzania. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kitayarishaji kama Mika Mwamba. Mika Mwamba ni mtayarishaji mashuhuri san  nchini Tanzania, na alijibebea umaarufu mkubwa sana nchini Tanzania kunako miaka ya 2000.

SOMA NA HII:  Ifahamu Simu ya Tecno S1 na Bei yake Nchini Tanzania

Miikka aliwahi kufanya kazi na wasanii mbalimbali wa nchini Tanzania. Wasanii hao ni: Dully Sykes, Inspector Haroun, Lady Jay Dee, Mad Ice, Chegge, Mandojo na Domo Kaya, Solid Ground Family, Complex, Zahrani (maarufu kama Big Punisher wa Bongo), Only Face, Dknob na wengine wengi .

Mika alihitimu shahada ya uzamili (MA) alipata Theatre Academy of Finland, Dept. of Light and Sound Design.

Licha ya kufanya kazi nchini kwa muda mchache sana kabla hajarudi kwao ulaya  aliacha historia ya ngoma zake ambazo zinasikilizwa mpaka hii leo, mfano mzuri ni ngoma ya , Julieta – Dully Sykes (2000), Baby Gal – Mad Ice (2002), Tupa Mawe – Zahrani na Complex (2001), Twenzetu – Chegge, Ferouz na Mh Temba (2005), Elimu na Mitaani.com – Dknob (2003) na bila kulisahau Kundi la Daz Nundaz.

 

HENRICO- SOUND CRAFTERS

Henrico ni mmoja ya watayarishaji wakongwe sana nchini ambaye ameweza kuibua vipaji vingi haswa kwa wasanii wa Temeke, Wasanii waliowahi kufanya kazi na Henrico ni kama Inspector Harun na kundi lake la Gangwe Mobb,Mabaga Fresh,Mack Malik Simba (R,I.P) ,Solo Thang na wengine wengi.

ROY WA G RECORD (R.I.P)- G RECORD

Enzi za uhai wake Roy alikuwa ni mmoja ya vichwa  kwenye utayarishaji wa midundo yenye ladha za upekee na utofauti mwingi, Roy ametengeneza nyimbo kama Mr Blue na wimbo wake Blue Blue na Enika -Baridi kama hii akiwa G. Records.

Baadaye  alitibuana na Dj Gulu au G-Love na kutengana, hivyo kwenda kuanzisha studio yake mwenyewe, G2 ambayo ilipata umaarufu baada ya muda mfupi tu.
Roy alikuwa producer gumzo na kipenzi cha wasanii wachanga, aliwainua wengi kama mmojawapo akiwa ni Matonya, Noorah mbali na Mr. Blue.

SOMA NA HII:  Swali la Siku: - Kati ya Vitu Hivi 3, Ni Kitu Gani Ni Ngumu Kwako Kuishi Bila Kukifanya?

Kabla ya G Records, Roy alikwishafanya kazi Sound-Crafters na aliwahi kurekodi wimbo wake mwenyewe, uliokwenda kwa jina la `Overnight’. Alishiriki pia kutayarisha albamu ya kwanza ya X- Plastaz.

SAID COMORIEN- METRO STUDIO

Comorien huyu alikuwa ni fundi wa vinanda, ukiwa ugonjwa wako ni vinanda basi tafuta ngoma alizotengeneza huyu mtu. Uwezo wake wa kukung’uta vinanda upo juu sana, sikiliza wimbo wa T.I.D wa nyota yangu usikie vile vinanda alivyoviingizia.Marehem Mez B (R.I.P) pia alishafanya kazi zake nyingi na Comorien bila kumsahau Noorah.

BONY LUV- MAWINGU STUDIO

Huwezi kuzungumzia historia ya disco nchini Tanzania na kuacha kumtaja DJ Bonny Luv . Ukifanya hivyo, wanaoielewa historia, ladha na utamu wa disco, enzi hizo lilipokuwa disco haswa, watakuona una lako jambo.

Bony Luv ni mmoja ya maproducer wa zamani ambao ni multi-talented ,anauwezo mkubwa wa kutengeneza ngoma,kufanya mixing kali na ku dj pia.Amefanya kazi na wakongwe wengi wa zamani likiwemo kundi la Kwanza Unit waliorekodi santuri ya kwanza kabisa iliyoenda kwa jina la Kwanza Unit mwaka 1993.

Hawa ni baadhi tu ya watayarishaji waliowahi kuvuma sana enzi hizo, lakini wapo wengine wengi kama Amit Mento alitengeneza ngoma nyingi kali zikiwemo vituko uswahilini original na remix ya Suma G aliyomshirikisha Inspekta Haroun, pia ndiye alimyemtoa pia Mez B na ngoma ya kwanza iliitwa Fikiria, alitengeneza ngoma nyingi.za TID kama, siamini,nk pia ngoma ya Ray C uko wapi na Kuna nyimbo kama mambo safi ya Marehemu Complex, Big Dog Pose BDP majobless,na kumwambia. Pia kulikuwa na watayarishaji kama Akili The Brain, Kameta na wengineo.


Sambaza:

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako