Nyingine

Tujadili: Ni Channel Gani Ya DSTV Huwezi Pitisha Siku Bila kuangalia?

DSTV, ni digital satellite TV service yenye umaarufu mkubwa barani Africa, Imeanzishwa mwaka 1995, inatoa huduma mbalimbali za kuvutia kama movie, maisha & utamaduni, michezo, documentaries, habari & biashara, muziki, Dini na channel zingine kwa MultiChoice subscribers.

Tangu kuanzishwa kwa huduma hii, imekuwa sehemu ya maisha ya watanzania kwa ubora wa stations zake  zinazofanya mtu awe na furaha muda wote anapoziangalia.

Sehemu ya burudani ya huduma hii ipo vizuri sana kwa sababu station zinazopatikana kwenye kipengele hiki zinawapa watumiaji burudani isiyo na kikomo kwanzia movies, muziki na nk.

Sehemu nyingine ni Sports, ina wanachama wengi ambao huwa hawafanyi kitu kingine chochote zaidi ya kuangalia TV hasa wakati kuna mechi ya timu wanazozipenda. Kwa wanachama ambao wako serious, kuna channels za kuelimisha zinazowaunganisha na masuala mbalimbali yanayohusu elimu.

Ndio, kwa wale wenye msimamo mkali wa dini , kuna stations mbalimbali ambazo hazina kitu kingine cha kuonyesha zaidi ya mambo yanayohusiana na dini, na upo huru kuchagua stations yoyote ile inayoendana na dini yako.

Nafikiri hakuna utakacho kikosa, ila ili TV yako iwe na mvuto unatakiwa kulipia ili kujiunga na huduma hizi.

Hata hivyo, mapenzi kwa binadamu hutofautiana ndio maana kitu unachokipenda zaidi mimi naweza nisivutiwe nacho kabisa. Wengi wanapenda michezo wakati kuna watu ambao mapenzi yao ni muziki au elimu, na pia kuna watu ambao hawawezi pitisha siku bila ya kuangalia movies.

Kwa wasomaji wetu waaminifu, kama una mpenzi na vituo vya DSTV, tuambie ni stations gani  huwezi pitisha siku bila kuangalia? Kuwa kweli na kumbuka kuacha maoni yako hapa chini.

Soma na hizi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Check Also

Close
Close