TTCL Kusimamia Njia Mpya ya Malipo kwa Wateja wa Mwendokasi


Shirika la huduma ya mradi wa mabasi yaendayo haraka DSM (UDART) limefanya marekebisho katika mfumo wa utoaji huduma na kwanzia leo Leo April 13, 2018 mfumo wa ukusanyaji nauli wa shirika hilo utakuwa chini ya Shirika la simu la Taifa (TTCL) badala ya kampuni ya Maxcom.

Njia mpya ya malipo kwa wateja wa Mwendokasi

Akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu mabadiliko hayo, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano, UDART, Deus Bugaywa amesema mkataba baina ya UDART na Maxcom umeisha baada ya kudumu takribani kwa miaka miwili kuanzia Mei 2016 hadi leo Aprili 14, hivyo wameamua kusaini mkataba mwingine na TTCL.

Pia Bugaywa amesema kuwa mabadiliko hayo yanaweza kusababisha usumbufu katika siku chache kuanzia sasa kutokana mfumo huo mpya wa TTCL.

“Nawaomba watumiaji wa usafiri huu wawe na imani kwani tunaamini mabadiliko haya yatakuwa ya kisasa,” -Bugaywa.
Kuhusu wafanyakazi waliokuwa wanatoa huduma katika vituo vya mabasi mabadiliko hayo hayatawaathiri, Bugaywa ameeleza wafanyakazi 191 waliokuwa wanafanya kazi kupitia Maxcom Afrika na kulipwa na UDART wataendelea na kazi na kubadilishiwa mikataba hivyo hawataathirika.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA