Sambaza:

Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kesho saa 7.00 itahitimisha mchakato wa kuzima huduma ya simu za mkononi zinazotumia teknolojia ya CDMA.

Mchakato huo ulianza kutekelezwa tangu Januari mwaka huu na unahitimishwa kesho usiku.

Kwa mujibu wa taarifa TTCL iliyotolewa na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu, Waziri Kindamba, ni kuwa uzimaji huo utaenda sambamba na kuwapatia wateja wao huduma mbadala kwa kutumia teknolojia ya 3G na 4G-LTE yenye ufanisi wa viwango zaidi.

Kampuni imeomba radhi kwa wateja wake kutokana na usumbufu utakaojitokeza na kuwataka wawasiliane na kituo cha huduma kwa wateja kilichopo karibu nao kwa msaada zaidi.

“Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza wakati wa zoezi hili linalolenga kuboresha huduma kwa wateja wetu,” amesema Kindamba kwenye taarifa hiyo.

Sambaza:
SOMA NA HII:  Fahamu Huduma za Timu ya Mwitikio wa Kukabili Majanga ya Kompyuta Tanzania

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako