TRL Yaanza Zoezi La Bomoa Bomoa Buguruni, DSM

Leo Jumamosi, Kampuni hodhi ya rasilimali za reli nchini (Rahco) imeanza kuvunja nyumba zaidi ya 250 zilizopo pembezoni mwa reli ya kati, kuanzia Stesheni hadi Pugu. Nyumba zilizobomolewa ni zile zote ambazo ziko ndani ya mita 30 kutoka kwenye Reli na zoezi hili linatarajiwa kuendelea Tanzania nzima kwa nyumba zote zilizo ndani ya hifadhi ya reli.

Wakazi wa eneo hilo wameilalamikia Serikali kwa kutotoa taarifa mapema jambo ambalo limesababisha baadhi yao kushindwa kuokoa mali walizonazao huku wengine wakiwa njia panda kwa kutofahamu ni wapi watalala.

 

Leave a Reply