Habari za Teknolojia

Reli na Treni za kisasa zazinduliwa Kenya ni kiwango cha “Standard Gauge”

Kenya imezindua reli mpya kati ya mji wa Mombasa hadi Nairobi ikiwa ni miezi 18 mapema.Reli hiyo iliotengezwa kupitia ufadhili wa shilingi bilioni 3.2 kutoka serikali ya China ndio mradi mkubwa wa miundo msingi kuwahi kutekelezwa na serikali tangu taifa hilo lijipatie uhuru wake.

Reli mpya ya SGR yazinduliwa Kenya

Mradi huo umechukua takriban miaka mitatu na nusu kwa kutumia teknolojia ya ujenzi wa reli ya China kukamilika.

Ni reli ya kwanza katika kipindi cha karne moja, pia inatarajiwa kuunganisha Sudan Kusini, DR Congo ,Burundi na Mombasa.

Safari ya kutoka Mombasa kuelekea Nairobi na treni ya kisasa itachukua saa nne na nusu ikilinganishwa na saa tisa kwa kutumia basi na saa 12 kwa kutumia treni ya zamani.

Kuhusu nauli ya Treni hizo kwa daraja la kawaida tiketi zitauzwa kwa Ksh 900 huku daraja la biashara nauli ikiwa ni Ksh 3000.Tazama picha za uzinduzi wa Reli hiyo ya kisasa na nyingine zinazoonesha kila kituo kutoka Mombasa hadi nairobi.

Behewa la Ist Class ambalo Wakenya watakaosafiria watalipa shilingi 3000

Rais Uhuru Kenyatta alisema maneno haya wakati wa uzinduzi wa reli hiyo ambayo imeanzisha mwamko mpya katika historia ya Kenya:

”Historia ilianzwa miaka122 iliopita wakati Waingereza waliokuwa wametawala taifa hili walipoanzisha treni hiyo iliokuwa haijulikani inakokwenda na kupewa jina Lunatic Express

”Leo licha ya kukosolewa pakubwa tunasherehekea Madaraka Express {ikitajwa baada ya siku ambayo Wakenya walijipatia uhuru wao kikamilifu} badala ya Lunatic Express.

Gharama ya mradi huo imekosolewa na upinzani ambao unasema mradi huo umeigharimu Kenya fedha nyingi mno. Vilevile wamemshutumu rais Kenyatta kwa kuomba fedha kutoka China bila mpango. Serikali nayo inasema kuwa ni sharti iwekeze katika miundo msingi ili kuvutia wawekezaji.

SOMA NA HII:  Mwongozo wa matumizi bora, sahihi na salama ya vifaa na mifumo ya TEHAMA serikalini

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako