Nyingine

TRA kupiga mnada nyasi bandia za timu ya Simba viongozi wa timu watoa neno

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imethibitisha kuwa nyasi bandia za klabu ya Simba zilizopo bandarini zitapigwa mnada endapo Simba watashindwa kulipa kodi wanayodaiwa.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo amesema Simba pia wananafasi ya kuzipata nyasi hizo endapo watalipa kabla ya tarehe ya mnada.

Makamu wa Rais wa Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amesema leo kwamba wana taarifa za mpango wa kupigwa mnada nyasi hizo na wapo kwenye mchakato wa kuzikomboa.

“Ni kweli kwa kawaida Bandarini kuna utaratibu, mzigo unapofika lazima ulipiwe utoke, ikishindikana hivyo unapigwa mnada. Kwa hiyo lazima tujitahidi tuzikomboe,”alisema.

Nae mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Ujenzi wa Uwanja Bunju Complex wa klabu hiyo, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba anashangaa kusikizia nyasi hizo bado hazijalipiwa, wakati fedha zilikwishapatikana.

“Unaponiambia hivyo ninashangaa, kwa sababu tulikwishafanya mpango fedha zikapatikana za kulipia hizo nyasi, sasa kuambiwa hazijalipiwa hadi sasa sijui ni kwa nini,”alisema Hans Poppe na kuongeza; “Ngoja niwasiliane na wenzangu, mimi nipo Kenya kwa sasa,”alisema.

 

Kwa upande wake Kampuni ya ya Udalali ya Majembe (Majembe Auction) wamesema kuwa watazipiga mnada endapo Simba watashindwa kulipa ushuru hadi kufikia tarehe ya mnada.

“Kampuni ya udalali ya Majembe Auction Mart inataka kupiga *mnada* nyasi bandia za SIMBA SPORTS CLUB na magoli yake, sababu kubwa ni uongozi (wamiliki) kushindwa kuzilipia *kodi*.

SOMA NA HII:  Je una bashiri "kubeti" ili kujikwamua na matatizo ya kimaisha ?

Mnada utafanyika Eneo la Nyuma ya “The Waterfront Sunset Restaurant and Beach Bar”, barabara ya Yatch Club, Masaki, ofisi mnada utakaofanyika zinaitwa *LW9*.

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako