Ifahamu Tovuti Inayokuwezesha Kutoa Taarifa za Unyanyasaji wa Watoto Tanzania


Tovuti ya kutoa taarifa ya IWF Tanzania inakuwezesha kuchukua hatua sahihi kwa kutuma picha na video kutoa taarifa unapoona unyanyasaji wa kingono kwa mtoto.

Taarifa yako inaweza kumuokoa mtoto muathirika kutoka katika unyanyasaji zaidi.

Kutoa taarifa ni kwa haraka na rahisi. Unaweza kutoa taarifa bila kujulikana. Na kama utapenda kujua hatima ya taarifa uliyoitoa, barua pepe yako itahitajika kwa lengo la kutumiwa hatima ya taarifa uliyoitoa.

Tafadhali kumbuka: Kama ungependa kutoa taarifa zaidi kuhusu mtoto aliyepo kwenye mazingira hatarishi au taarifa nyingine yoyote tofauti na picha au video za ukatili wa kingono, tafadhali wasiliana na dawati la polisi karibu na wewe au piga simu namba 116, Huduma kwa Mtoto.

Unaweza Kutoa taarifa kwa urahisi kwa kutembelea tovuti ya IWF Tanzania

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA