Top 3 Bora ya Android Security Apps Zinazoweza Kurahisisha Maisha Yako!


Leo kwenye Mediahuru [dot] Com, nataka nikushirikishe na wewe baadhi ya programu bora za usalama za android (android security apps) kwenye Google Play Store. Lakini kabla ya kuelezea baadhi ya pointi zangu, kwanza tujadili baadhi ya maswali ambayo unaweza kuwa nayo kuhusu mada hii.

android security apps

“Kwa nini natakiwa kuwa na programu ya usalama ya android kwenye simu janja yangu ya Android?”

“Ikiwa ni muhimu sana, ni programu gani bora za usalama kwenye android app directories?”

Maswali mazuri!

Napenda kujibu haraka kwa ajili yenu.

Kwanza, hebu tuzungumze kuhusu kwa nini unatakiwa ku-install kwenye simu janja yako baadhi ya programu bora za usalama za android kwenye Google Playstore.

Katika dunia ya leo, malware na wizi wa simu janja vimekuwa vitu maarufu sana, na kama mtu hajawa makini, kuna uwezekano wa hackers kushambulia kwa urahisi na kufanya udukuzi kwenye simu yako kwa ku-install malware.

Kwa kweli, hackers hawana mpango na simu yako ya kisasa au jinsi ilivyo ghali,  lakini badala yake wanavutiwa na kuiba taarifa zako za siri na zenye umuhimu zaidi kwako.

Pia, unaweza kupoteza simu yako kwa sababu ya kutoijali kwa sehemu yako mwenyewe au labda kwa sababu ya kuibiwa na watu wengine wasiojulikana mitaani. Bila shaka, huna mamlaka ya kichawi ya kurudisha simu yako.

Sasa, hizo ni baadhi ya sababu zinazofanya uwepo umuhimu wa kuinstall programu ya usalama ya android kwenye simu janja yako ya android.

Kwa kuwa tumeweza kuthibitisha ukweli na sababu za kwanini unatakiwa kutumia android security apps kwenye simu zako za mkononi, hebu tuangalie baadhi ya programu za usalama ambazo ni bora zaidi kwenye playstore.

3 Bora ya Android Security Apps Mwaka 2018

1: CM Locker

Programu hii ni dhahiri moja ya programu bora za usalama kwa sasa, ina chaguzi nyingi sana, hasa katika maeneo ya muonekano na utendaji.

Interface yake ya kipekee kwa mtumiaji ni ya kuvutia sana!

android security apps

Zaidi, ina screen-lock na app locker ambayo inasaidia kulinda data zako dhidi ya wata wenye nia mbaya.

Mbali na kulinda data zako za siri (confidential data) kwa kufunga screen ya simu yako, pia inalinda simu yako dhidi ya wezi, inaweza kukusaidia kujua simu uliyopoteza ipo sehemu gani.

Huwezi kuamini, lakini pia ina utendaji wa Intruder Selfie (Intruder Selfie function) ambao unapiga picha ya watu ambao huingiza password isiyo sahihi kwenye simu janja yako ya Android.

Pakua sasa kutoka:

2: Avast Mobile Security

Nafikiri tayari unaifahamu vizuri programu ya “Avast” antivirus.

Hii ni programu ya antivirus iliyotumiwa na watumiaji wengi wa Windows OS na mimi pia naitumia kwenye kompyuta yangu ya HP.

Kile inachofanya ni rahisi, ina scan mafaili yote na programu kwenye pc yako kuangalia kama kuna malware. Itakapo kutana na masuala yoyote yanayo sumbua kwenye faili zako, mara moja hutoa onyo “Virus has been detected”.  Kisha moja kwa moja ina repair au kufuta malware kwa niaba yako.


Ni kama hivyo tu, Avast Mobile Security inalinda simu janja yako dhidi ya virusi na programu hasidi (malware) zinazosababisha popups na matangazo yasiyohitajika. Pia, programu hii ya usalama wa android inakupa taarifa unapo install spyware na adware apps zinazovunja faragha yako.

Kitu kingine kinachofanywa na programu hii ya usalama wa simu ya android kwa ajili yakoni ni kusaidia kulinda vifaa vyako dhidi ya mashambulizi ya uharibifu kutoka kwenye barua pepe, simu, tovuti zilizo ambukizwa au hata ujumbe wa SMS.

Baadhi ya Sifa Zake:

 • Antivirus Engine
 • Call Blocker
 • Anti-Theft
 • Photo Vault
 • Power Save
 • App Locker
 • Privacy Permissions
 • Firewall (for rooted Android only)
 • Charging Screen
 • RAM Boost
 • Junk Cleaner
 • Web Shield
 • WiFi Scanner
 • WiFi Speed Test

Niamini mimi, programu hii ina uwezo mkubwa sna wa kulinda na kuboresha uzoefu wako wa kutumiaji mfumo wa Android.

Pakua sasa kutoka:

3: Cheetah Mobile Security Master

Programu hii ni mojawapo ya programu bora za usalama wa android kwenye Hifadhi ya Google Play, na ufanyaji wake wa kazi unashangaza!

Hii ni programu ambayo imefungua ukurasa mpya wa usalama wa simu kwa sababu hailinda simu yako tu bali inahifadhi faragha yako.

CM Security app, tofauti na programu nyingine za usalama za android , ina chaguo la kulinda simu zako za mkononi kwa kufanya diagnosing na kukushauri juu ya ufumbuzi muhimu kama vile; antivirus, junk clean, na pone booster (battery saver, na CPU cooler) kwa wakati.

android security apps

Kipengele kingine cha kuvutia kwenye CM Security app ni ulinzi wa faragha kupitia kuunda ngao kwa shughuli zote za mtandaoni kupitia SafeConnect VPN.

Kwa kweli, Cheetah Mobile’s Security Master naipata asilimia 100 kwa real-time detection na asilimia 100 kwa kugundua programu zisizofaa (malware) zilizopatikana katika wiki nne zilizopita katika ripoti ya karibuni ya AV-Test. Pia haina athari ya kutumia sana nguvu betri au utendaji wa simu janja yako.

Pakua sas kutoka:

Mwisho

Hizo ni baadhi ya zinazotumika zaidi na bila shaka ni programu bora za usalama kwenye android kwenye Google Play Store, na nadhani ni bora zaidi ukizitumia kusafisha na kulinda simu janja yako ya Android dhidi ya malware, spyware, au hata adware.

Unapaswa kupakua programu yoyote ya usalama ya Android niliyotaja hapo juu, na utanishukuru baadaye!

Je, una programu bora zaidi katika akili yako?

Tuambie kupitia sehemu ya maoni!

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA