Sambaza:

Magari ya gharama kubwa zaidi duniani yana mambo mengi zaidi ya kuwa usafiri. Sanaa iliyotumika kutengeneza magari haya ni ya kipekee duniani, upekee wake na mikogo ni baadhi ya vitu vinavyofanya yawe na thamani ukiacha utendaji wake wa kazi na ufanisi uliotumika kuyatengeneza. Katika maisha yetu ya kila siku magari haya hushangaza wengi na hapa napenda kushare nawe list ya magari 10 yenye thamani zaidi Duniani.

Kwa ufafanuzi tu, nimeweka magari yaliyotengenezwa hivi karibuni, ambayo tayari yapo barabarani kisheria-unaendesha bila ya kujali – na nimeacha magari classic yanayouzwa kwenye mnada. Pia nimepunguza orodha kuwa na nameplate moja, hivyo usitegemea kukuta gari tano tofauti za Bugatti Veyron kwenye list.

SOMA NA HII:  Ifahamu ndege kubwa zaidi inayoweza kutua kwenye maji

1.  $4.8 million — Koenigsegg CCXR Trevita

 

Koenigsegg inashikilia nafasi ya kwanza na gari aina ya CCXR Trevita, ni gari ya gharama kubwa zaidi duniani. Kwa nini inavunja benk yako kiasi hicho? , gari hili limenakshiwa na madini ya almasi…na almasi sio bei rahisi.

2. $4.5 million — Lamborghini Veneno

Gari hili limetengenezwa kuadhimisha miaka 50 ya kampuni hiyo ya utengenezaji wa magari, mwonekano wake una navutia kila pande, jinsi lilivyo unaweza kusema si la dunia hii- sioni ajabu kuuzwa $4.5 million.

3. $3.4 million — W Motors Lykan Hypersport

Utakumbuka Lykan Hypersport imetumika kwenye movie ya Furious 7. Sio Dominic Toretto pekee anayefaidika na uwepo wa gari hili, jeshi la polisi la Abu Dhabi linatumia Hypersport kwenye  doria zake  ingawa inatumika kwajili ya masoko na mahusiano ya umma tu.

SOMA NA HII:  Magari 5 Maarufu Kwenye Movie na Uwepo Wake kwa Sasa

4.  $3.4 million — Limited Edition Bugatti Veyron by Mansory Vivere

List hii isingekamilika bila ya kuwepo na toleo hata moja la Bugatti Veyron. Gari hili sio tu ni moja ya magari yenye kasi zaidi duniani bali ni gari  lenye gharama kubwa pia.

5. $3 million — Ferrari Pininfarina Sergio

Ikiwa na thamani ya  $3 million, Ferrari Sergio sio gari lenye thamani zaidi kwenye list yetu ila ni gari ambalo sio rahisi kulimiliki hata kama una hela kwa sababu ni magari sita tu yalitengenezwa.

6. $2.6 million — Pagani Huayra BC

SOMA NA HII:  Kufikia 2040 China itakuwa imefikia hatua hii ya teknolojia ya magari

7. $2.5 million – Ferrari F60 America

8. $2.5 million — Bugatti Chiron

9. $2 million — Koenigsegg One:1

10.  $2 million — Koenigsegg Regera

Sambaza:

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako