Sambaza:

Karibu tena kwenye safu yetu ya kila wiki  Top 10 Android App Updates , ambapo tunaangalia programu/apps nyingi zilizoboreshwa wiki hii. Tumegundua kwamba moja ya njia bora ya kugundua programu muhimu ni kutafuta zile ambazo zimefanyiwa update na waendelezaji (developers) badala ya kuchagua programu/app zilizo pakuliwa zaidi.

Kama ilivyokuwa hapo mwanzo, tutafafanua masasisho madogo kwenye programu zinazojulikana sana ambazo zimepakuliwa zaidi ya mara milioni 10, lakini tutaongeza baadhi ya app ambazo zimekuwa na masasisho muhimu lakini bado hazijawa na watumiaji wengi. Tunatarajia utafurahia kipengele hiki cha kila wiki ndani ya Mediahuru na utakutana na baadhi ya programu ambazo zina muhimu.

HTC Edge Sense – Version Varies

Kitu gani kipya kwenye toleo hili:

 • Visual feedback style mpya
 • Ina support HTC Alexa

WhatsApp Messenger – Version 2.17.254

Kitu gani kipya kwenye toleo hili:

 • Unaweza kutuma faili la aina yoyote. Unaweza kutuma  document, chat, Bonyeza attach — document.
 • Kutoka kwenye kamera ya ndani ya app, sasa unaweza kusogeza kuona picha na video zako zote.
 • Wakati wa kuandika maandishi katika chat, unaweza kugonga na kushikilia ili kuchagua maandishi yawe bold, strikethrough, ama italicize.
 • Maboresho mbalimbali yamefanyika kwajili ya call za sauti na video.

Skype – Version 8.1.0

Kitu gani kipya kwenye toleo hili:

 • Udhibiti(controls) mpya umeongezwa ili kusaidia watumiaji kusimamia vibration na LED notification alerts.
 • Tatizo la kutoonekana kwa shortcut icon ya Skype limefanyiwa kazi
 • Maboresho mengine yamefanyika kwenye PSTN call.

Astro: AI Meets Email – Version 2.0.4

Kitu gani kipya kwenye toleo hili:

 • Picha na attachment: Sasa unaweza kuongeza picha kutoka kwenye kamera yako ya ndani.
 • VIPs: Ikiwa mtu hana umuhimu sana, nenda kwenye Mipangilio (setting) ili kuondoa VIP
 • Bug fixes

Google Play Games – Version 5.2.0

Kitu gani kipya kwenye toleo hili:

 • Adaptive icons (Android O)
 • Notification channels (Android O)
 • Data backup (Android 6.0+)
 • Smaller apk

Kitu gani kipya kwenye toleo hili:

 • Unatafuta kitu cha kufanya katika VR? Angalia maudhui bora zaidi na uzoefu katika mtazamo kwenye Daydream iliyotengenezwa upya.
SOMA NA HII:  Ushauri wa Obama kuhusu matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii
 • Angalia controller yako wakati unapokuwa Daydream Home, Quick Settings au Play Store kwenye VR; Vitufe vya kubonyeza sasa vimesisitizwa.
 • Utendaji wa Controller umeboreshwa. Ni mambo madogo.

TuneIn Radio – Version 18.1.0

Kitu gani kipya kwenye toleo hili:

 • TuneIn sasa ina mwonekano mpya !
 • Bug fixes, crash fixes na maboresho mengine.
 • Tatizo la podcast kukatika karibu na dakika 30 na kuanza kurudia sasa limerekebishwa.

TickTick – Version 3.8.0

 

TickTick

Kitu gani kipya kwenye toleo hili:

 • “Time Duration” sasa inaunga mkono kufanya kazi zaidi ya siku moja. Unapoweka tarehe zote mbili ya kuanza na kumaliza kazi , Unaweza kwa urahisi kuboresha mwonekano na kupata maelezo ya wazi ya kazi zote kupitia  Calendar View.
 • Mandhari mpya ya mji wa Seoul inapatikana kwa watumiaji wa premium.
 • Wakati idadi ya orodha za kawaida inazidi tatu, basi zitakusanywa kwenye folda moja.

 

Google Keep – Version 3.4.803

 

Google Keep

Kitu gani kipya kwenye toleo hili:

 • Imeongezwa vibonyezo vya undo/redo kwenye bar ya chini.

 

Journey – Diary, Journal – Version 1.23.1

Journal

Kitu gani kipya kwenye toleo hili:

 •  Weather service mpya (WeatherBit)
  – Historia ya hali ya hewa hadi mwaka 1
  – Icons mpya za hali ya hewa
  – “Single location viewer” mpya
  – Tatizo la kichwa cha habari kwenye WordPress limefanyiwa kazi


Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako