Apps za Simu

Top 10 Android App Updates Wiki Hii: Deezer, YouTube,Firefox

on

Karibu tena kwenye safu yetu ya kila wiki  Top 10 Android App Updates , ambapo tunaangalia programu/apps nyingi zilizoboreshwa wiki hii. Tumegundua kwamba moja ya njia bora ya kugundua programu muhimu ni kutafuta zile ambazo zimefanyiwa update na waendelezaji (developers) badala ya kuchagua programu/app zilizo pakuliwa zaidi.

Kama ilivyokuwa hapo mwanzo, tutafafanua masasisho madogo kwenye programu zinazojulikana sana ambazo zimepakuliwa zaidi ya mara milioni 10, lakini tutaongeza baadhi ya app ambazo zimekuwa na masasisho muhimu lakini bado hazijawa na watumiaji wengi. Tunatarajia utafurahia kipengele hiki cha kila wiki ndani ya Mediahuru na utakutana na baadhi ya programu ambazo zina muhimu.

Android Samba Client – Version 1.1.0

Kitu gani kipya kwenye toleo hili:

 • Imeongezwa SMBv3 support

Adobe Lightroom – Version 3.0.0

Kitu gani kipya kwenye toleo hili:

 • Angalia interface ya mtumiaji ambayo imeundwa kutoka chini!!
 • Ina-support kamera za hivi karibuni na lenses zinazopatikana kwenye toleo la ACR 9.12 (orodha kamili ya kamera na lenses zinazofanya kazi kwenye Lightroom inapatikana kwenye http://www.adobe.com/go/supported_cameras)
 • Maboresho ya jumla ya utulivu wa App

Slacker Radio – Version 7.12.2

Kitu gani kipya kwenye toleo hili:

 • Sleep timer? Nzuri. Siku zote nilikuwa natamani iwee na sleep timer.

Nintendo Switch Parental Controls  – Version 1.1.1

Kitu gani kipya kwenye toleo hili:

 • Angalia maelezo zaidi ya kucheza (play details) – Muda wa kucheza na programu zilizochezwa sasa zinaweza tazamwa tofauti kwa kila mtumiaji wa Nintendo Switch. Pia, pata taarifa kila programu mpya inapopakuliwa.
 • Angalia taarifa za mwezi kwa ufupi- Idadi ya siku na muda unaweza kutazamwa kwa kila mtumiaji. Unaweza kushirikisha (share) muhtasari kwa kutumia kibonyezo cha share.
 • Zima kengele – Kipengele hiki kinazima kengele za muda wa kucheza kwa siku unayotaka mtoto wako kucheza kwa muda mrefu.

YouTube for Android TV – Version 1.3.11

Kitu gani kipya kwenye toleo hili:

 • Imeongezwa chaguo (option) ya kujiunga na channels.
 • Updates kurasa za channel.
 • Chaguo jipya kwenye orodha ya mipangilio (settings menu) ikiwa ni pamoja na kipengele cha “stats for nerds”.
 • Bug fixes mbalimbali.

Firefox Focus – Version 1.1.0

Kitu gani kipya kwenye toleo hili:

 • Angalia video zikiwa full screen kutoka kwenye tovuti mbalimbali za video
 • Ina-support downloads
 • Maboresho kwenye “notification actions”  ili kufungua haraka Firefox Focus kupitia njia ya notifications.

Deezer – Version 5.4.8.46

Kitu gani kipya kwenye toleo hili:

 • Muziki kwenye vidole vya mkono – Muda upo upande wako linapokuja swala la muziki, hasa sasa ambapo unaweza kufungua na kutumia Deezer kwa kutumia Android Wear.
 • Jipya kwenye kurasa ya msanii – Kugundua albamu zilizo na msanii nje ya discography zao wenyewe.
 • Laini kama vile magurudumu ya Chrome – Deezer imeimarishwa kwenye Chromecast kwa kurekebisha baadhi ya bugs.

Tasker – Version 5.0.0

Kitu gani kipya kwenye toleo hili:

 • Imehamia kwenye Material Design icon na themes
 • Imeboresha usambazaji na ushirikiano wa UI
 • Imeongeza material design icons karibu 900, zikiwa na uhuru wa kuchagua rangi
 • Zimeongezwa themes nne zaidi kwenye Prefs / UI / Theme
 • support ya (customisable) Quick Settings (Android 7.0+) na App Shortcuts (Android 7.1.1+)
 • Video scene element ikiwa na udhibiti mzuri.

Google Express – Version 18.0.0

Kitu gani kipya kwenye toleo hili:

 • Usaidizi wa orodha ya ununuzi nje ya mtandao ipo hapa! Fikia/angalia orodha yako yote ya ununuzi wakati huna intaneti.
 • Ongeza, ondoa na uhariri listi ya vitu ukiwa hujaunganishwa na mtandao na mabadiliko yako yote yatakuwa synced utakapoingia kwenye mtandao.
 • Taratibu za duka na usafirishaji wa bidhaa zimeboresha, hivyo chaguo la “pick substitutions” limeondolewa.
 • Furahia mchakato mpya wa kujiunga ili kufanya manunuzi kwa haraka.

ZOOM Cloud Meetings – Version 4.0.365

Kitu gani kipya kwenye toleo hili:

 • Chat setting kwajili ya webinar hosts imebadilishwa.
 • Chaguo msingi la sasa hosts wanaruhusu washiriki kuzungumza (chat) na “all panelists and attendees.”
 • Masuala mbalimbali yametatuliwa
 • Minor bug fixes
SOMA NA HII:  Tumia camera kupiga selfie, unapata majibu ya saratani

 

About Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Leave a Reply

Your email address will not be published.