Toleo jipya la Microsoft Surface Pro yenye 4G LTE kuzinduliwa Desemba 1


Kama ilivyotabiriwa mwezi wa Septemba, Microsoft imetumia tena mkutano wake wa Mwaka “Future Decoded ” uliofanyika London kutambulisha vifaa vingine vipya. Leo, kampuni hiyo imethibitisha kuwa itazindua Surface Pro mnamo Desemba 1 yenye uwezo wa LTE.

Panos Panay, VP wa kampuni ya Microsoft kwa vifaa vya Windows, ametoa tangazo hilo. Alisema kuwa kifaa hicho kipya kinachojulikana kama Microsoft Surface Pro kina “LTE Advanced”, itaanza kupatikana kwanza kwa wateja wa kibiashara.

Kifaa hiki kinajumuisha Intel Core i5 CPU na Qualcomm Snapdragon X16 modem. Inaweza kutumike katika nchi yoyote ile, hii inafanya kiwe kifaa sahihi kwa wale wanaosafiri sana. Aidha, Microsoft imeongeza kuwa kasi ya kupakua itaweza kufikia 450 Mbps.

Kampuni hiyo haikusema chochote kuhusu uwezo wa betri kwenye bidhaa zake mpya. Inadhaniwa kuwa uwezo wa LTE utapunguza masaa 13.5 ambayo watu wanaotumia toleo la Wi-Fi la Surface Pro wanayapata, ingawa bado haijulikani ni kiasi gani .

Toleo la msingi la Microsoft Surface Pro yenye LTE Advanced, ambayo inakuja na 4GB ya RAM na 128GB SSD, itakuwa na bei ya $ 1149. Toleo lenye uwezo mara mbili zaidi wa RAM na uhifadhi itakuwa na bei ya $ 1149.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA