Habari za Teknolojia

Ifahamu Timu ya Mwitikio wa Kukabili Majanga ya Kompyuta Tanzania TZ-CERT

TZ-CERT ni kifupisho cha Tanzania Computer Emergency Response Team, timu ya kitaifa yenye wajibu wa kuratibu mwitikio wa matukio ya usalama wa kimtandao katika ngazi ya Taifa na kushirikiana na vyombo vya kikanda na vya kimataifa vinavyoshughulikia udhibiti wa matukio ya usalama wa kimtandao.

TZ-CERT ilianzishwa chini ya Kifungu 124 cha Sheria ya Elektroni na Posta (EPOCA) Na. 3 ya 2010 ndani ya mfumo wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

TZ-CERT iko ndani ya muundo wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)

JE, TZ-CERT INAFANYA NINI?

Lengo kuu la CERT ya Taifa ni kuwa na usalama wa hali ya juu na wa uhakika ndani ya nchi; na kujenga utamaduni wa usalama wa mtandao na taarifa kwa manufaa ya jamii (serikali, wananchi, walaji, biashara na asasi za sekta ya umma) na hivyo kuchangia utendaji kazi usio na vikwazo wa shughuli zinazoendelea mtandaoni.

 1. Inatoa fursa ya kutoa taarifa ya matukio ya usalama wa kompyuta yatakayopitiwa na kushughulikiwa.
 2. Inasambazaa taarifa za matukio muhimu yanayohusu umma.
 3. Inaleta utambuzi wa usalama wa mtandao.
SOMA NA HII:  Drones kutumika kuwafukuza wafanyakazi kazini

Dira ya TZ-CERT ni kuwa kiungo kinachoaminiwa duniani kote cha kushughulikia matukio ya kiusalama wa mtandao.

Ina dhamira ya kuboresha na kuunga mkono msimamo wa taifa kuhusu usalama wa mtandao, kuratibu ushirikiano wa taarifa na kwa makusudi kusimamia mashaka ya mtandao wakati huo huo kusaidia ahadizawashirika.

JE, NI MATUKIO GANI YA MARA KWA MARA YA USALAMA WA KOMPYUTA?

Linaweza kuwa tukio la kweli au linalotuhumiwa lenye madhara kuhusiana na usalama wa mifumo ya kompyuta au mitandao ya kompyuta katika kukiuka wazi wazi au kudhaniwa kukiuka sera ya usalama wa kompyuta. Matukio hayo yanaweza kujumuisha shughuli kama vile :

 1. Kujaribu kuingia bila idhini kwenye mfumo au data zake
 2. Kukatiza kusikotakiwa au kunyimwa huduma
 3. Kutumia mfumo kusikoidhinishwa kwa ajili ya kuchakata au kuhifadhi data
 4. Kubadili vifaa vya mfumo, programu tumizi zinazodhibiti na kusimamia, au sifa bainifu za programu tumizi bila ya idhini, taarifa au maelekezo ya mmiliki.
SOMA NA HII:  SNORT mfumo wa bure wa Kugundua Kuvamiwa na Kuzuia

NI NANI WATATOA TAARIFA ZA MATUKIO YA USALAMA WA KOMPYUTA?

Washirika wa TZ-CERT, watu au taasisi ambazo TZ-CERT imekusudiwa kuwahudumia au kuwasaidia ambao ni pamoja na :

 1. Serikali
 2. Miundombinu muhimu ya TEHAMA
 3. Ulinzi na Usalama
 4. Taasisi za fedha na benki
 5. Taasisi za kitaaluma
 6. Wananchi kwa jumla
SOMA NA HII:  Marekani Inasema Korea ya Kaskazini Inahusika na Mashambulizi ya WannaCry

Je, utatoaje taarifa ya matukio kwa TZ-CERT?

Matukio yanaweza kutolewa taarifa kwa TZ-CERT kupitia :-

Fomu ya utoaji taarifa ya tukio : www.tz-cert.go.tz
Barua pepe : incidents@tzcert.go.tz
Simu : +255 22 2412039
Faksi : +255 22 2412038

Ofisi za TZ-CERT ziko wazi kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa saa 2 asubuhi hadi 10 jioni. Unaweza kuuliza maswali na kutoa mapendekezo yako kupitia barua pepe yao info@tzcert.go.tz

Chanzo
https://www.tzcert.go.tz/
Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako