Habari za Teknolojia

Tigo Tanzania kushirikiana na SportPesa

on

KAMPUNI ya mitandao ya simu za mkononi ya Tigo Tanzania, imekuwa mshirika rasmi wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa, tangu juzi Jumamosi.

Ushirika huo una maana kuwa sasa wateja wanaotumia Mtandao wa Tigo watapata nafasi ya kucheza na SportPesa kama ilivyo kwa mitandao ya Vodacom na Airtel.

Akizungumzia juu ya ushirika huo mpya, Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya SportPesa, Tarimba Abbas, alisema: “Hii ni nafasi nzuri kwetu na kwa wateja wa Tigo kwani tulikuwa tunapokea maombi mengi juu ya uhitaji wao wa kushiriki kucheza na SportPesa kama ilivyo kwa mitandao mingine.

SOMA NA HII:  Mbinu za Kubeti Mpira wa Miguu na Kushinda

“Wateja wa Tigo wanatakiwa kutuma neno GAME kwenda namba 15888 ili kujisajili, mtumiaji wa mtandao wa Tigo ili aweze kucheza na SportPesa anatakiwa kuanza kwa kuweka pesa kwenye akaunti yake ya SportPesa kwa kupiga namba 15001#, kuchagua malipo ya bili, kuweka namba ya biashara ambayo ni 150888, kuingiza namba ya kumbukumbu ambayo ni neno SPORTPESA kisha ataweka kiasi pamoja na namba ya siri ili kumaliza kujisajili.”

Ushirika na Tigo umekuja wakati muafaka ikiwa ni wiki mbili tu tangu kampuni hiyo ambayo ni wadhamini wa klabu za Simba, Yanga na Singida United kutambulisha promosheni yake mpya ijulikanayo kama RAFIKI BONUS ambapo wateja wa SportPesa wanapata fursa ya kuwaalika marafiki zao kujisajili na kucheza na SportPesa ili wao waweze kujipatia kiasi cha shilingi elfu mbili za Kitanzania kwa kila rafiki anayejiunga na kucheza na SportPesa.

SOMA NA HII:  Wema Sepetu na Jokate ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii #Tanzania Heritage Month

Kwa taarifa zaidi wanaweza kutuma neno rafiki kwenda 15888.
Wateja wa SportPesa wanashauriwa kupiga simu za huduma kwa wateja 0764115588, 0658115588 na 0692115588 kwa taarifa zaidi kuhusu bonasi ya rafiki na huduma mbalimbali zitolewazo na kampuni hiyo.

Kwa maswali, tafadhali wasiliana nao kupitia:
Idara ya Masoko, SportPesa Ltd.
P.O. Box 23315, Dar es Salaam
Simu: 0746 233 599
Email: marketing.TZ@sportpesa.com
www.sportpesa.co.tz
Instagram: @tzsportpesa
Twitter: @TZSportPesa
Snapchat: sportpesatz
Facebook: www.facebook.com/SportpesaTZ/
Namba za huduma kwa wateja: 0764115588 / 0658115588 / 0692115588

About Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published.