Sambaza:

Katika mwendelezo wa juhudi zake za kuboresha huduma kwa wateja wake nchini, Tigo leo imezindua duka jipya na la kisasa Jijini Dodoma.

Duka jipya ya Tigo jijini Dodoma lipo kwenye jengo la CDA, barabara ya Uhindini, mkabala na mzunguko wa magari wa CDA.

Akifungua duka hilo la kipekee jijini Dodoma, Kaimu Meneja Mtendaji wa Tigo Tanzania, Bw. Simon Karikari alisema kuwa duka hilo jipya linaleta huduma zote za Tigo chini ya mwavuli mmoja.

Duka hilo lina eneo ya wageni mashuhuri (VIP section) na wale wanaohitaji huduma za haraka, kaunta nyingi zaidi za kuhudumia wateja pamoja na sehemu ambayo itawawezesha wateja wapya kujaribu bidhaa na huduma bora za Tigo kama vile simu za kisasa na Tigo pesa.

SOMA NA HII:  Mfahamu Mchekeshaji wa miaka 7 kutoka Nigeria aliyefika Hollywood

Tigo inaelewa mahitaji ya wateja wake na imejizatiti kuhakikisha kuwa wateja wote wanapokea huduma bora, za haraka na uhakika kwa viwango vya kimataifa katika maduka yake 52 yaliyoenea nchi nzima.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Kaskazini – George Lugata, Duka hilo jipya la Tigo lenye uwezo wa kuhudumia wateja 300 kwa siku litakuwa wazi kila siku za wiki.

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako