Baada ya kashfa thamani ya facebook yashuka kwa $58bn


Mmiliki wa mtandao wa kijamii wa facebook, Mark Zuckerbag aliomba msamaha kufuatia ukiukaji wa sheria ya data ulioathiri zaidi ya watu milioni 50 lakini bado mtandao huo wa kijamii unakabiliwa na hisia kali kutoka kwa wanasiasa , wawekezaji na wateja wake kufuatia kashfa ya data.

Wawekezaji wengi wanajiuliza ni kwa kiwango gani uharibifu huo utaathiri mtandao huo wa kijamii, baadhi ya wawekezaji wamegoma kuuza hisa zao huku taarifa mbaya zilizotokana na kashfa ya Cambridge Analytica zimefanya watangazaji wengine wa matangazo kusema ‘Imetosha’.

Hisa katika mtandao huo wa kijamii zilianguka kutoka $176.80 siku ya Jumatatu hadi $159.30 siku ya Ijumaa jioni. Hisa za facebook ziliuzwa kwa $38 kila moja na hivyobasi kuipatia kampuni hiyo thamani ya kibiashara ya $104b. Kufuatia ukuwaji thabiti na utawala katika matangazo ya kidijitali hisa za facebook zilipanda hadi $190 kufikia Februari mwaka huu.

Kampuni ya matangazo ya Mozilla na Commerzbank siku ya Jumatano ilisitisha kwa muda matangazo yake katika mtandao huo wa facebook. Siku ya Jumatano kampuni ya kiteknolojia Elon Musk ilifutilia mbali kurasa za kampuni zake za Telsa and Spaces.

Je, unaamini hisa za facebook zitajinusuru na kuimarika? Je unaamini taarifa iliyotolewa na mwanzilishi wa facebook itasaidia kuboresha mtandao huu wa kijamii? Toa maoni yako.

 

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA