Home Nyingine TENGENEZA MALENGO YA KUKUFIKISHA KATIKA NDOTO ZAKO.

TENGENEZA MALENGO YA KUKUFIKISHA KATIKA NDOTO ZAKO.

0
0

Malengo ni mawazo ambayo umedhamiria kuyafikia! Lakini pia malengo ni mafanikio ya baadaye yaliyopangiliwa yenye muda ukomo ambayo unaenda kuyafanyia kazi! Malengo ni mwongozo wako wa kufikia malengo yako! Ni mahali ambapo unataka kupafikia! Hebu angalia unaenda mahali ambapo hupajui! Ooh balaa hii! Kuwa na malengo ni jambo la msingi sana katika maisha! Ni kitu ambacho kina hamisisha katika maisha vinavyoweza kukufanya ukue na kufikia malengo yako!

NAMNA YA KUANDIKA MALENGO BINAFSI!

Jiulize swali kabla ya kuanza kuandika malengo, jiulize unataka nn maishani mwako?

Hatua za kuandika malengo!

1.Angalia mambo unayoyapenda kuyafanya au kuyafikia!

Fikiria miaka michache nyuma uliwaza nn? Ulitaka kuboresha nn? na kubadili nn?

Mambo haya yatakuwa msingi wa malengo yako! Uwe na malengo unayoyafikia kwa muda ili kutimiza!

Yagawe ktk vipengere vidogovidogo mfano maisha binafsi, afya, uchumi, kazi na hata uwekezaji wako! Mfano orodhesha nn unataka kukipata kupitia taaluma yako, ajira yako hata ktk uchumi! Andika uwekezaji wako!

2.Weka vipaumbele!

Baada ya kuorodhesha malengo yako, sasa anza kuweka vipaumbele. Yapange malengo yako kwa kuangalia vipaumbele! Huwezi kuyafanya mambo yote kwa wakati mmoja! Angalia nn cha kwanza kukifanya!

Yagawe malengo yako katika sehemu tatu!

Malengo ya jumla – malengo ya mhimu zaidi!
Malengo ya kati- ni yale ambayo yanakuja kiasili.
Malengo ya mwisho/ madogo.

3.Anza kuyafanyia kazi malengo yako.

Kila siku hakikisha unafanya jambo fulani kutekeleza malengo! Fanya kitu fulani kwa ajili ya malengo yako! Mfano-kufanya utafiti, kutafuta maarifa, kuhifadhi pesa. Punguza baadhi ya mambo yanayopelekea kupoteza mambo mengi! Kama unataka kuwa mkulima anza kupata maarifa kuhusu kilimo!

Kama unataka kuandika kitabu punguza muda wa kulala, tafuta vielelezo na materials zinazoendana na kitu unachotaka kukiandika!

4.Tengeneza tarehe au muda wa mwisho! Deadline!

Kuwa na orodha ya malengo unayotaka kuyafikia bila kuweka muda/ tarehe ya ukomo ya kukamilisha hutafika mbali! Angalia orodha yako na tengeneza mbinu za kila siku zinazoendeleza malengo yako!

Mfano unataka kuwa umenunua shamba kufikia mwaka 2022! Au uwe na kiasi fulani cha fedha kufikia mwaka 2020! Tengeneza ratiba ya siku, wiki na mwezi ya mambo unayotaka kukamilisha kufikia malengo! Weka kalenda ya kufanya kila jambo kuelekea malengo! Tarehe ya ukomo inakuwajibisha! Kadri muda unavoendelea ndivyo unavoongeza kuwajibika kufikia malengo! Kama huna deadline utakuwa unafanya kizembe na kwa kuahirisha mambo!

5.Tengeneza mipango mikakati!

Mipango mkakati ni orodha ya matendo yatakayo kuongoza kufikia malengo! Tengeneza na weka mfululizo wa hatua utakazozipitia! Weka hatua gani utakazozichukua kufikia hapo! Mikakati yako ipangiliwe kwa mtiririko mzuri! Fikiria njia nzuri inayowezekana kuelekea malengo! Pangilia utaanza na nn na utamaliza na nn? Utafanyanye kufika hapa! Yaandike yote kwa ufasaha mkubwa!

6.Anza na lengo kuu la kwanza!

Tambua hatua ya kwanza kuchukua! Ni bora kuanza na hatua moja ya msingi na anza kujenga mwanzo mzuri wa kuelekea malengo! Kama lengo lako la kwanza ni kujenga anza leo kuchukua hatua za ujenzi, anza Leo kuweka akiba, jenga wazo akilini mwako utafanyaje kukamilisha! Kama lengo lako ni kuwa mwanasheria anza kufatilia nn cha kufanya ili uwe mwanasheria! Kama ni kuwa mwanamziki mkubwa anza kujifunza walau instrument moja, tafuta role model, tafuta sifa zake nzuri! Tafuta maarifa yanayoendana na kitu hicho! Usiache siku ipite bila kufanya jambo kufikia malengo! Ondoa vipingamizi vilivyopo akilini mwako. Jiandae kwenye imani binafsi zinazokuzuia au kukutatiza! Ondoa mawazo ya kushindwa kabisa! Chukua majukumu ya maisha yako! Jenga shauku ya kile unachokitaka! Passion! Kuwa na hamu ya kile utakacho kukifanya!

Mwisho naweza kumaliza kwa kusema kuwa malengo na matarajio vinafanana japo sio jambo moja! Malengo ambayo hayajaandikwa ni matarajio! Na matarajio sio malengo! Kama hujaandika basi hayo ni matarajio! Huwezi kuishi kwa kutegemea matarajio/ wishes!

Ni bora kuwa na malengo yaliyoandikwa na yahifadhi kadri uwezavyo! Tafuta notebook inayotunzika! Waweza kuhifadhi kwenye email yako! Ukiwa na malengo yatakufanya ufikie mafanikio yako! Hakuna mafanikio yasiyo na malengo! Malengo makubwa mafanikio makubwa!

LEAVE YOUR COMMENT

Your email address will not be published. Required fields are marked *