Teknolojia ya hali ya chini au juu ni mkombozi kwa mamilioni ya watu – WFP


Teknolojia iwe ya hali ya chini au ya hali ya juu imekuwa mkombozi kwa mamilioni ya watu wenye uhitaji wa aina mbalimbali, kuanzia wakimbizi hadi wakulima limesema shirika la mpango wa chakula duniani WFP.

Kwa mujibu wa Robert Opp, mkurugenzi wa idara mpya ya ubunifu na mabadiliko ya utawala WFP, teknolojia ni muhimu sana kwa operesheni za usaidizi wa kibinadamu za umoja wa Mataifa.

Idara yake ndio iliyounda Apu ya Share The Meal inayosaidia kulisha mamilioni ya wakimbizi katika sehemu mbalimbali duniani. Na ameongeza kuwa  wakati mwingine si lazima iwe ya kiwango cha juu na sio kwa wakimbizi pekee

(SAUTI YA ROBERT OPP )

“Kwa mfano kufanya kazi na wakulima wadogowadogo 250,000 Afrika Mashariki  kwa kuwapa vihenge vilivyolipiwa sehemu ya ruzuku ambavyo ni teknolojia ya hali ya chini  pamoja na mafunzo, ili kuwawezesha kuhakikisha kwamba mavuno yao  hayaharibiki kwa sababu yamehifadhiwa vizuri.”

Na kwa wakimbizi wanaohitaji msaada kwa udi na uvumba amesema wanatukia teknolojia za aina tofauti ikiwemo ya hali ya juu mfano

(SAUTI YA ROBERT OPP)

Mfumo wa malipo wa kidijitali nchini Jordan kuwafikia wakimbizi wa Syria na msaada kupitia mfumo wa vocha za kidijitali ambazo ni haki ya kifedha, wanaweza kwenda kwenye duka lolote wanalotaka katika ukanda huo na kuweza kununua bidhaa za chakula kwa kutumia mfumo huo”

Amesema hivi sasa mashirika mengi ya misaada yanageukia teknolojia kwani inarahisisha kazi yao na kuwafikia watu wengi zaidi.

Makala hii imenakiliwa kutoka tovuti ya Umoja wa Mataifa

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *