Sambaza:

Katika kuunga mkono juhudi za Serikali kuleta maendeleo kwa wananchi kampuni ya magari ya Mantrack Tanzania imeendesha warsha fupi kwa lengo la kutambulisha vifaa na teknolojia mpya itakayoongeza ufanisi wa kazi hasa katika sekta ya ujenzi.

Teknolojia mpya katika sekta ya Ujenzi

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwakilishi wa Mantrack Tanzania alisema wana lengo la kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuhakikisha Tanzania mpya inajengwa na uchumi bora kutokana na miundombinu bora.

”Vifaa hivi ni imara na vinatumia teknolojia mpya ya kisasa inayosaidia utendekaji wa shughuli za ujenzi kuwa rahisi. Tumeamua kuja na kasi ya Serikali mpya ya kutenda vitu kwa urahisi na kwa ufanisi wa hali ya juu.”

Warsha hiyo imefanyika katika Karakana ya Mantrack Tanzania karibu na Jengo la Quality Plaza, Barabara ya Nyerere na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa ujenzi.


Sambaza:
SOMA NA HII:  TANESCO yaanzisha mfumo mpya wa kulipia Bill

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako