Nyingine

Teknolojia 5 Maarufu kwenye Magari Kwa Sasa

2018 inakuja na kwa madereva wanaopenda teknolojia kwenye soko la gari mpya, Mwaka Mpya unamaanisha vifaa – gadgets mpya. Magari hivi sasa yanazidi kuwa ya kisasa, na wakati ubora wa gari, usalama na uwezo wa kutumia mafuta ni baadhi ya vitu ambavyo vipo juu kwenye orodha za umuhimu ya wanunuzi, teknolojia iliyotumika ni moja ya sababu kuu za kuuza gari haraka.

Magari

Teknolojia inaweza kuwa na msaada inapoongezwa  kwenye gari, lakini vipengele vya usalama lazima viwe juu kwenye orodha ya  kila mmiliki wa gari. Vitu kama “premium stereos, heated seats,na automatic parallel parking” ni vizuri kuwa navyo. Vipengele vya usalama vinavyomsaidia dereva na kuwa faida kwa kila mtu kwenye barabara vinapaswa kupewa kipaumbele cha juu. Vitu vingine vinaweza kuzingatiwa baadaye.

Hapa chini nimekusogezea vipengele 5 vya teknolojia ambavyo unaweza kuvizingatia wakati wa kununua gari jipya mwaka huu na kuweka kila mtu salama barabara.

SOMA NA HII:  Swali la Siku: - Kati ya Vitu Hivi 3, Ni Kitu Gani Ni Ngumu Kwako Kuishi Bila Kukifanya?

1. Imeunganishwa na Apps ya Simu Janja

Simu za mkononi kwa kiasi kikubwa zimebadilisha njia za madereva za kuingiliana na magari yao. Wakati watengenezaji wengi wa magari kwa sasa wanatoa aina fulani ya programu inayounganishwa na smartphone, ni bora kufanya utafiti ili kupata iliyo sahihi zaidi kwako.

Apps zinazowezesha wamiliki wa magari kufunga na / au kufungua gari zao huku wakiwa mbali ni nzuri kwa mahitaji ya ziada ya usalama. Pia kuna app za simu za mkononi ambazo zinawasaidia madereva muda wote kujua vitu kama vile kiwango cha mafuta, oil, na upepo kwenye tairi. Baadhi ya programu zinaweza hata kuwasha gari kwajili yako.

2. 360° Camera

Je! Umewahi kutaka kuwa na macho nyuma ya kichwa chako? Hii unaweza kuipata kwenye gari lako.

Mfumo wa kamera 360 ° unaweza kufanya maisha kuwa rahisi sana kwa madereva kwa sababu ajari zingine hutokea wakati wa kufanya maegesho. Kuniwa na kamera kila upande wa gari, pamoja na mfumo wa kisasa wa kompyuta, ni sawa na dereva mwenye ujuzi zaidi. Madereva wanaweza kupata msaada wa thamani kwa kuona mazingira yanayozunguka gari. Ukiwa na mfumo wa kamera ya 360 °, kazi kama vile kuegesha gari kwenye maegesho yenye magari mengi inakuwa rahisi sana kufanyika.

3. Mfumo wa dharura wa breki (Automatic Emergency Braking)

Wakati madereva wanapaswa kuwa na ufahamu wa barabara wanayopita, haina madhara kuwa na msaada mwingine, kwa tahadhari zaidi. Pamoja na sensors mbalimbali mahali, Automatic Emergency Braking au AEB ni kimbilio la mwisho inapotokea ajari.

Kama jina lake linavyoonyesha, automatic emergency braking itafunga breki moja kwa moja ili kuepuka mgongano. Kipengele hiki cha usalama ni kizuri mno, lakini madereva wanapaswa kukumbuka kuwa automatic emergency braking sio mbadala wa pedili za breki. Ni chombo cha manufaa kwa madereva ambao hawawezi kusimamisha gari kwa haraka iwezekanavyo tatizo linapotokea mbele yao.

Itakapofika mwaka 2022, Automatic Emergency Braking itakuwa kitu cha kawaida kwenye magari yote. Hii ni pamoja na Audi zote, Mercedes Benz, Ford, BMW, Toyota, General Motors, Mazda, Tesla, Volkswagen, na Volvo zilizouzwa kwa umma.

Kwa bahati nzuri, madereva hawapaswi kusubiri mpaka ufike mwaka huo ili kupata mfumo wa dharura wa breki. Wazalishaji wengi wa gari tayari watengeneza magari yenye mfumo huu wa dharura katika baadhi ya magari yao ya hivi karibuni.

4. Lane Departure Warning

Wakati mwingine madereva hutoa kipaumbele zaidi juu ya kile kinachotokea kwenye kiti cha nyuma na kutoa kipaumbele kidogo kwenye barabara. Kila mtu jambo hili limewaahi kumtokea kwa namna moja au nyingine. Na pale tunaporudisha macho yetu kwenye barabara tuonakuta gari ilianza kuingia kwenye njia isiyo sahihi.

“Lane departure warning” ni kipengele cha usalama ambacho kinapaswa kupunguza viwango vya ajari zinazotokana na kutokuwa makini kwenye barabara.Mfumo huu unatumia kamera kuamua ikiwa gari inatembea nje ya mstari.

5. Wireless Charging

Kuwa na waya wa kuchajia simu kwenye gari haivuti kabisa. Kwa bahati nzuri, magari mengi zaidi na zaidi yamefungwa “wireless charging pads”. Kwa kuwa na wireless charging pads, swala la kuwa na chaja ya kawaida ni swala la kizamani. Madereva wanaweza kuzingatia zaidi masuala yanayoendelea barabarani huku simu zao zikiendelea kuchaji na abiria hawatakuwa na wasiwasi

Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako