Simu za Mkononi

Tecno Spark K7 VS Infinix Hot 5 Lite Simu Gani Bora Zaidi ?

Si habari tena kwamba Tecno Mobile watengenezaji wa smartphone za Tecno hivi karibuni ilizindua mfululizo mpya wa smartphones zenye bei nafuu zilizopewa jina la Tecno Spark na kwa upande mwingine Infinix, moja ya mshindani mkubwa wa Tecno kwenye uwanja wa simu pia hivi karibuni alizindua toleo la Lite la Infinix Hot 5 katika mfululizo wao wa Hot series.

Katika makala ya leo, tutajumuisha mojawapo ya mfululizo mpya wa Tecno Spark, Tecno Spark K7 na kuzungumzia uwezo wake kwa kulinganisha na Infinix Hot 5 Lite.

Simu hizi mbili Tecno Spark K7 na Infinix Hot 5 Lite zina sifa nyingi zinazofanana, kwanzia ukubwa sawa wa skrini na display resolution hadi ukubwa wa ROM / RAM na zote zina bei sawa kwenye soko, kwa hivyo utakubali kwamba vifaa hivi viwili vinafanana sana.

Ulinganisho kati ya Tecno Spark K7 na Infinix Moto 5 Lite utakusaidia kufanya uchaguzi wako kati ya vifaa hivi ikiwa unafikiria kununua moja yapo.

SOMA NA HII:  Tecno Camon C8 vs Tecno Boom J8 – Ninunue simu gani ?

Bila ya kuongeza maneno zaidi, hapa chini ni picha za maelezo ya ulinganisho kati ya Tecno Spark K7 na Infinix Hot 5 Lite X559.

Simu zote mbili, Tecno Spark K7 na Infinix Hote 5 Lite kwa sasa hupatikana katika maduka makubwa ya wafanyabiashara wa simu na wanauza Tsh 200,000.

Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako